Friday, September 18, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ

Wape shavu A.Y, Shaa
Tuzo za MAMA (MTV Africa Music Awards) zipo on air na inajulikana kwamba hapa Bongo, Ambwene Yesaya ‘AY’ na Sara Kaisi ‘Shaa’ ndiyo nominees pekee waliotajwa kushiriki.

A.Y anachuana na wakali kama Jigga, Kanye West katika tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop, Shaa anaparurana na wasanii wa mataifa mengine katika tuzo ya Msanii Mpya Bora.

Wanaweza kushinda ikiwa tu hautobana kuwapigia kura, kumchagua AY andika neno BHH AY kwenda namba 0789 777 333 na Shaa unaandika BNA SHAA kwenda namba 0789 777 333. Unaweza kupiga kura mara nyingi kadiri uwezavyo ili kuipa heshima Tanzania katika eneo la muziki.
******** *******************************

IJUMAA SEXIEST BACHELOR: Ray, Makamua- Big Out
Last week, Ray, Makamua na Chid Benz walikuwa katika mstari wa hatari a.k.a mguu ndani mguu nje, lakini leo kuna majibu ya waliokwenda nje ya shindano.

Kwa mujibu kura za wasomaji wetu, Ray na Makamua ndiyo mastaa wanaoaga shindano, hivyo kubakiza majina 10 ya mastaa ambao wanaendelea kuwania taji la Ijumaa Sexiest Bachelor 2009-2010.

Hata hivyo, Chid Benz anaendelea kubaki kwenye mstari wa hatari, hivyo kama si kura yako wewe msomaji, kijana ataaga shindano.

Unachotakiwa kufanya ni kuandika ujumbe mfupi wa maneno, SMS kupitia simu yako ya mkononi, unaandika neno IJUMAA unaacha nafasi, halafu unaandika namba ya mshiriki kisha unaituma kwenda namba 15551.

Mfano; IJUMAA 00 halafu unaituma kwenda namba 15551.
**************************

Product ya Bongo ndani ya mjengo wa Big Brother Africa Revolution, Elizabeth Gupta, amesema kuwa atakuwa wa mwisho kutoka nyuma ya washiriki wote, Chile Kasoga anashuka nayo.

Eliza ambaye alikuwa ni contestant wa Miss Tanzania 2008-09 na kuliacha taji kwa Nasreen Karim alisema kuwa anaamini kuwa atatimiza siku 91 ambazo ndizo watakaofika fainali Big Brother Revolution watakaa kabla ya yeye kubaki wa mwisho.

Mtizedi huyo aliyasema hayo wakati akijitambulisha kwa washiriki wenzake wa kike mjengoni ambapo alisema kuwa anaamini kuwa siku ya fainali atakabidhiwa briefcase yenye noti za US Dollar 200,000 ambazo ni karibu sawa na madafu 260,000,000.

Alisema: “Nitakuwa kivyangu kwa muda wote wa siku 91, nitahakikisha nalinda heshima yangu kikamilifu.”
*******************************************

Chegge Chigunda
Kutoka pande za TMK, mchizi ambaye anaedelea kusimama vyema ndani ya Kundi la Wanaume Family, Said Juma a.k.a Chegge Chigunda au Mtoto wa Mama Said, amesema na ShowBiz kwamba kupitia programu inayoendelea ndani ya gazeti ndugu na hili, Risasi anajiandaa kupata mke wa maisha yake.

Msanii huyo (picha juu) alisema kwamba programu hiyo yenye jina la ‘Shinda kuwa mke wa Chegge’ imemkutanisha na wasichana wengi lakini anaamini atampata mmoja ambaye ni mwema. Kupitia programu hiyo msichana ambaye atashinda kuwa mke wa Chegge atatajwa wiki ijayo.

Hivi sasa Chegge amesimama na ngoma mbili, hewani, Karibu Kiumeni aliyomshirikisha Ngwea na Running Low remix aliyogonga na Wahuu wa Kenya, siku kadhaa zijazo ataachia kali nyingine, aliyompa shavu Lady Jaydee, unajua ni ipi? Kaa tayari.
******* ********************************
Compiled by mc george

No comments: