Friday, September 4, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

VUMI na ukweli kuhusu game yake
Kwa mara ya kwanza tangu alipopata umaarufu kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, msanii anayekuja kwa kasi ya ajabu, Vumilia Abraham a.k.a ‘Vumi’ amedondoka ndani ya ShowBiz na kupiga stori mbili tatu kuhusiana na sanaa yake.

Ndani ya safu hii, mwanadada huyo alisema kuwa muziki ndio maisha yake kitu kinachomfanya anapotinga studio atulize kichwa ili kutoka na ngoma za ukweli.

Vumi ambaye kwasasa anasumbua na albamu yake moja inayokwenda kwa jina la ‘Utanikumbuka” alidai kuwa, ameweka muziki mbele akiamini siku moja taaluma hiyo itamtoa kimaisha.

“Nauchukulia muziki kama sehemu muhimu ya maisha yangu, ndio maana niingiapo studio nakaza buti kinoma ili niweze kutoa kitu cha uhakika kitakachokubalika kwa mashabiki wangu,”alisema Vumi.

Aidha, msanii huyu, ambaye ni tunda la THT, bado anaamini muziki bila shule ni bure na kwamba ameamua huku akifanya muziki awe pia anapiga buku akitambua kuwa shule itamsaidia kufanya mambo yake kitaalamu zaidi.
*********

mtoano wiki ijayo
Kupitia hapa safari ya Ijumaa Sexiest Bachelor 2009-2010 ndiyo kwanza imeanza, wiki hii hatutakuwa na mshiriki anayeaga shindanoni bali tunatoa nafasi nyingine kwako wewe mpenzi wa ShowBiz ili uendelee kutuma kura yako ukilitaja jina la mmoja ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi.

Sina haja ya kuzitaja sura na majina ya hao 12 waliyofanikiwa kuanza rasmi shindano kwani kila mmoja anaonekana wazi. Unachotakiwa ni kuandika jina la mshiriki mmoja na kulituma kwenda simu namba 0787 110 1173 au 0713-355 717, kura yako ndiyo mwamuziki na jaji wa shindano hili.

Kumbukeni kwamba, mpambano huu unaletwa kwenu chini ya udhamini wa Zizzou Fashion wauzaji wa pamba za kijanja kupitia maduka yao yaliyopo Sinza Afrika Sana na Victoria, Dar es Salaam. Mbali na mdhamini huyo mpambano bado unahitaji wadhamini wengine ambao wataufanya uwe bora zaidi. Cheki na sisi kupitia namba hizo juu.
***********

Isinika: Alishindwa mume wangu itakuwa wao!
Kutoka ndani ya Bendi ya muziki wa dansi, African Stars ‘Twanga Pepeta’ ShowBiz ilidondoshewa ishu mpya kutoka kwa mwanadada Janeth Isinika anayeshika maiki ndani ya wana wa kutwanga hao ambaye alisema kwamba watu wengi wamekuwa wakishangaa kwanini ameamua kuwa taiti na muziki wakati yeye ni mrembo mwenye sifa zote za kuolewa.

Akifafanua kuhusu hilo, mwanamuziki huyo alisema kuwa muziki ni sanaa aliyoipenda tangu alipokuwa mdogo na kwamba hawezi kushawishiwa na mtu yeyote kuachana na game hiyo mpaka pale atakapoamua mwenyewe na inawezekana akapiga kazi hiyo mpaka mwisho wa maisha yake.

“Napenda watu waelewe kwamba, kama niliweza kuachana na mume wangu kwakuwa hakutaka niendelee kuimba muziki wao watawezaje kunishawishi niachane na sanaa hiyo. Niliupenda muziki tangu nilipokuwa mdogo na yeye alinikuta kwenye muziki iweje anikataze kufanya kitu ninachokipenda?” Alihoji msanii huyo ambaye huwavutia wanaume wengi hasa anapokuwa jukwaani.
******

*********************************

Halle Berry na mimba nyingine!
Akiwa na umri wa miaka 43 sasa, staa wa muvi na mitindo huko pande za Hollywood, Marekani, Halle Berry anatarajia kupata mtoto wa pili baada ya kutundikwa mimba na mwanamitindo mwenzake Gabriel Aubry ambaye ni ‘boyfriend’ wake.

Rafiki wa karibu na Halle aliuambia mtandao mmoja unaodili na ishu za mastaa wa kiwanja kuwa staa huyo na mpenzi wake, Gabriel wamefurahia kupatikana kwa mimba hiyo ya pili ukizingatia kwamba mtoto wao wa kwanza, Nahla, walimpata kwa tabu.

“Kutokana na hilo wawili hao wameamua kuzaa tena na kuhakikisha wanafika kwa daktari ili kumpata mtoto wao wa pili kwa njia salama. Mtoto Nahla alipatikana kwa taabu sana hivyo mtoto huyo kwao ni kama muujiza waliopewa na Mungu, wamefurahi,” alisema rafiki huyo.
**********
compiled by mc george

No comments: