Ikiwa imekirudisha kwa kasi kile kipengele cha waliyopotea ‘Mwana Mpotevu’, mwishoni mwa wiki iliyopita ShowBiz ilienda hewani pande za Mwanza na kupiga stori na binti aliyewahi kufanya maajabu kunako miaka ya 2000 kupitia game ya muziki wa kizazi kipya huku akiwa na umri mdogo.
Anaitwa Pendo Farida Koshuma a.k.a Farida, kama humkumbuki vizuri, ukitajiwa majina ya ngoma kama Upendo wa mama, Pesa na nyingine, utagundua kwamba binti huyo kitambo alipotea tangu alipodondosha albamu yenye jina la ‘Upendo kwa mama’.
Akipiga stori na ShowBiz, Farida ambaye hivi sasa anamiliki age ya miaka 24 amesema kuwa, alisepa kwenye game baada ya kubanwa na masomo, lakini sasa anarudi upya akiwa ni mama wa mtoto mmoja wa miezi 8 na mwenye jina la Dominatha Kindole, huku akiwa ametia sauti yake isiyochuja kunako ngoma ya msanii Philbert Kabago ambaye alikuwa memba wa Kundi la SWV lenye maskani yake jijini Mwanza.
“Unajua hata kipindi kile nafanya muziki mwaka 2000, nilikuwa nasoma kidato cha pili, baada ya kukamilisha albamu yangu nikaamua ‘kuji-kipu’ bize na masomo mpaka hivi karibuni nilipohitimu katika Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa nilipokuwa nachukua Sheria. Kwa hiyo mbali na muziki hivi sasa natafuta kazi kama msomi,” alisema Farida.
Ndani ya ngoma hiyo ya Kabago yenye jina la Wivu, mrembo huyo ameonesha uwezo wa nguvu kitu ambacho kimeifanya ShowBiz iamini kuwa bado yuko fiti. Kwa upande wa Philbert ambaye pia ni mtangazaji wa kituo kimoja cha redio pande hizi, alisema kwamba aliamua kumshirikisha Farida ili kuleta tofauti katika kazi zake ikiwa ni ‘projekti’ ya albamu mpya.
*********************************
MLELA "Natamani kuchana lakini sauti sina"Kutoka pande za Kinondoni, Dar es salaam, staa wa muvi za Kibongo mwenye cheo cha ‘Ijumaa Sexiest Bachelor’ Yusuph Mlela a.k.a Angelo amesema na ShowBiz kwamba mbali na kugonga filamu anahusudu sana game ya muziki, lakini tatizo linakuja kwenye sauti, Samirah Phillip alipiga naye stori.
Ndani ya safu hii, juzikati Mlela alitamka ishu hiyo baada ya kuulizwa ni sanaa gani nyingine anaikubali mbali na kuigiza. Pia mchizi alisema kwamba angekuwana sauti ya ukweli tayari angekuwa ameshagonga singo kadhaa kama siyo kudondoka na albamu.
“Lakini pamoja na yote nawaheshimu sana wanamuziki wa Kibongo wanaoendelea kufanya vyema kila kukicha, nawakubali sana,” alisema Mlela huku akimalizia kwamba ushindi wa Ijumaa Sexiest Bachelor unaendelea kumuweka juu kila jua linapochomoza kwa kumfanya aongeze idadi ya dili ikiwemo kupiga matangazo ya makampuni mbalimbali huku mtaani heshima ikiongezeka mara dufu.
*****************************
Benjamini, A.T Wamefulia
Yale maoni tunayoendelea kuandika karibu kila wiki kupitia hapa kuhusiana na kuporomoka kwa game ya muziki wa kizazi kipya yanaonekana kuanza kuleta changamoto kwa wasanii wa muziki huo ambao wengi wameanza kufanya kazi za ukweli zinazoashiria kuwarudisha vizuri kunako mradi huo.
Baadhi yao ni vijana wawili, Benjamini wa Mambo Jambo na A.T kutoka Uswazi Records ambao kazi zao ziko poa ile mbaya. Kama bado haujafahamu ni ngoma zipi nazizungumzia, ‘Nimefulia’ ambayo Benja kampa shavu msela huyo wa Uswazi, huku ‘Nipigie’ ya A.T na Stara ikionekana kuanza mwaka vyema.
Kama wasanii wote wataamua kuumiza vichwa na kufanya kazi za ukweli huku wakipata sapoti ya kutosha kutoka kwa wadau mwaka huu unaweza kuwa wao baada ya kupoteza mwelekeo kwa kipindi kirefu.
1 comment:
Kila mtu anafanya kile roho inapenda. Namzimia sana Yussuf Mlela katika kazi zake lakini tatooos No!!!!!
Post a Comment