Fella na briefcase la mwaka wa fedha 2010
Meneja mshika MIC wa TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa’ ametua briefcase lenye maelezo kuhusu programu za kazi na fedha kuhusu yeye na kundi lake kwa mwaka wa fedha 2010-2011. Mkubwa alidondosha program hiyo kwa Abby Cool & MC George over the weekend ambayo tunaichambua kama ifuatavyo:
1.Kumtoa Said Juma ‘Chege’ na albamu yake, inayoitwa Karibu Kiumeni. 2.Ipo albamu ya kundi, inayoitwa Wanaume Kazini. 3.Analipa gharama za albamu ya qaswida, ya Madrasat Salama Islamiah, iliyopo Mbagala. 4.Atawatoa Amani James Temba a.k.a Mheshimiwa na Chege katika mradi wa pamoja, albamu yao inaitwa Vita Mbele. 5.Amefungua studio ya kurekodi Audio ambayo inaitwa Poteza Records. 6.Mwisho anaelekeza nguvu kwa underground, mwaka huu amejiwekea mkakati wa kumtoa mmoja wa kiume.
Kifo cha Bongo Fleva
Yap, ni mjadala kuhusu kifo cha kibudu cha Bongo Fleva. Huko nyuma tumepitia maeneo mbalimbali ambayo kwa maana moja au nyingine yamesababisha muziki huo ambao ulikuwa umeanza kung’ara, kubadili uelekeo na kushika njia ya kaburini.
Baada ya kugusa maeneo hayo, leo tunageukia studio za uchochoroni a.k.a studio uchwara, hizi kwa kiasi kikubwa zimesababisha Bongo Fleva ishike kasi kwenye njia ya kaburini.
Iko hivi, wakati watu wapo serious, wanafanya kazi za ukweli, kuna watu fulani kwa kufuata mkumbo, wakaona kumbe nao wanaweza kufanya biashara. Wakafungua studio na kuanza kutoa rekodi mbuzi.
Enzi zile anavuma Enrico na Sound Crafters, P. Funk na Bongo Records, Master Jay na MJ Production, Miika Mwamba na FM Studio, mara tukasikia Mbagala Charambe nako kuna studio. Heee!
Watu wakaona dili kwa sababu mzuka wa Bongo Fleva ulikuwa juu, watoto bila kujua quality ya muziki, wao wakawa wanalipa mkwanja, wanaingia chumba cha sindano, wanaingiza vocal baada ya nusu saa, mixing tayari anakabidhiwa mzigo kwenye CD.
Studio uchwara wakawa wanapata dili nyingi kwa sababu chaji yao haikuwa kubwa.
Wakati watu serious walitoa ngoma ikiwa na kiwango kwa shilingi 200,000 wakati huo, kule uchochoroni kuna track zilifanywa mpaka kwa wekundu watatu (30,000).
Tatizo kubwa likaja, washkaji baada ya kukabidhiwa CD, wakapeleka redioni. Zile redio serious zikagoma kucheza nyimbo hizo ambazo ni chafu katika quality ya muziki, lakini kule kwa ma-DJ na watangazaji njaa, ngoma zilichezwa na matokeo watu wakaanza kuchoka.
Zipo track mbovu masikioni, zilizorekodiwa ambazo ziliingizwa kwenye chati fulani fulani, kisa eti, msanii alikata mpunga kwa DJ au mtangazaji wa program husika. Taratibu muziki ukaanza kushuka thamani. Hao waliorekodi kwa kiwango duni, wakatengeneza albamu, wakampelekea mdosi ambaye hajui quality ya muziki, akaanza kuuza, matokeo yake akajaza nyimbo nyingi zisizokuwa na kiwango mtaani.
Kutokana na kuwa na kazi nyingi, mdosi akaanza kudengua, akipewa kazi na watu serious, anapanga bei ya chini. “Vevee iko kama hutaki kwenda bana, hapa ipo na kazi nyingi.”
Ikafikia kipindi, wasanii wakali wakabanwa, maprodyuza serious wakapungukiwa na kazi. Walikuwa wanafanya kazi usiku na mchana, lakini ikawa mchana ni miayo tu, wasanii hawaendi kurekodi.
Mtu ana Mic moja, kompyuta moja, mixer ya disko vumbi, keyboard ya bei chee kwa wamachinga wanaopitisha barabarani, eti naye anamiliki studio. Anarekodi. Ni wengi sana wameuroga muziki huu.
Rocky City: Wasanii kukwea ‘level’ nyingine
Tabia ya wasanii wengi wa Rocky City a.k.a Zoo au ukipenda unaweza kuita Mwanza, kukimbilia Dar, imepata dawa! Abby Cool & MC George over the weekend inatonya kuwa pande hizo za Kamanda Jamal Rwambow, imefunguliwa bonge ya studio.
Studio hiyo ya audio, ina kiwango cha kimataifa, hivyo badala ya wasanii kukimbilia Dar au Nairobi kutafuta studio zenye ubora, wanaweza kufanya kazi ‘babkubwa’ Zoo na zikachezwa kwenye vituo vya redio vya kijanja.
Studio hiyo inakwenda kwa jina la ATP na inapatikana pande barabara ya Rufiji jijini humo, na Meneja wa Studio hiyo, Iku Mwakisambwe, alisema nasi kwamba lengo ni kupandisha kiwango cha wasanii wa Rocky City ili kikubalike kimataifa.
Mastaa ambao tayari wameingiza voko kwenye studio hiyo ni Dark Master, Geez Mabovu, Z- Anto, Bwana Misosi, Chelea Man na wengine. Hey, Jitaman, H. Baba, Fid Q, Hard Mad, Rado na wengine, mnaweza kufikiria kurudi nyumbani?
JenniferLove
Aanza ngono akiwa na miaka 14, ametoa uroda kwa njemba 24
Ebwana Dah! Staa wa muvi, Jennifer Love Hewitt ndiye anaye take cover kwenye safu hii na hapa inatajwa orodha ya njemba ambazo kwa nyakati tofauti amezikabidhi penzi lake.
Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti inayodili na ishuz za uhusiano wa mastaa wa mbele kwenye eneo la nani kamrukia nani, Jennifer Love alianza kuchangamkia sanaa ya kitandani akiwa na umri miaka 14 tu. (Aliwahi sana).
Scott Bairstow ndiye kidume anayetajwa kuanza kuchangamka naye mwaka 1994 ambapo Jennifer alikuwa na umri wa miaka 14. Akaja Joey Lawrence ambaye alichangamsha damu kwa mwaka mmoja, 1995 – 96, akiwa na miaka 15.
Alipotoka kwa Joey, Jennifer kwa mtindo wa bandika bandua, alijiweka kwa Will Friedle ambapo penzi lao lilidumu kuanzia mwaka 1996 – 97 kabla kuamua kuutua mwili wake kwa Andrew Keegan, 1997.
Penzi la Jennifer na Andrew lilidumu kwa muda mfupi mno na baada ya kutoka kwake alihamishia majeshi kwa Carson Daly kuanzia mwaka 1997 – 99.
Hata hivyo, akiwa na Carson, Jennifer ‘alichiti’ na kumgea kidogo Jeff Timmons mwaka 1998. Mwaka 1999 alijipumzisha kwa muda kwa Diego Serrano kabla ya mwaka huo huo kutuliza mizuka kwa Rich Cronin ambaye alikaa naye mpaka mwaka 2001.
Kwa mara nyingine, Jennifer akiwa na Rich, mwaka 1999 ‘alimchiti’ na kumegana kisela na Wilmer Valderrama, pia mwaka 2000 kwa Alec Baldwin.
Aidha, mwaka 2000 huo huo, alianzisha uhusiano na Craig Bierko na kudumua naye mpaka mwaka 2001. Hii inamaana kuwa mbali na ‘kuchiti’ mara kwa mara kwa watu tofauti, pia kati ya kipindi cha mwaka 2000-01, Jennifer alikuwa na wanaume wawili permanent, Craig na Rich.
Mwaka 2001-02, Jennifer alijiweka kwa Patrick Wilson, pia mwaka 2001, hakuona soo kumpa penzi lake Enrique Iglesias, mwaka 2002, alimegana na Shaggy, mwaka huo huo akajikunja na John Mayer, na kuanzia mwaka 2002-03, alimchagua Paul Nicholls. Baada ya hapo, Jennifer akajiweka kwa John Cusack, hiyo ilikuwa ni mwaka 2003, mwaka huo huo akajikunja na Stephen Dorff, Kip Pardue, Antonio Sabato na Scott Austin ambaye walimwagana mwaka 2004.
Mwaka 2004, alijiweka kwa Will Estes, mwaka uliofuata, hapo unazungumziwa 2005, alikaa kwa Ross McCall ambaye walitosana mwaka 2009 na baada ya hapo akahamia kwa Jamie Kennedy ambaye yupo naye mpaka sasa.
Jennifer, alizaliwa Februari 21, 1979, Waco, Texas, Marekani, kwahiyo ana umri wa miaka 30.

*************************************************

*******************************************************
Rocky City: Wasanii kukwea ‘level’ nyingine
Tabia ya wasanii wengi wa Rocky City a.k.a Zoo au ukipenda unaweza kuita Mwanza, kukimbilia Dar, imepata dawa! Abby Cool & MC George over the weekend inatonya kuwa pande hizo za Kamanda Jamal Rwambow, imefunguliwa bonge ya studio.
Studio hiyo ya audio, ina kiwango cha kimataifa, hivyo badala ya wasanii kukimbilia Dar au Nairobi kutafuta studio zenye ubora, wanaweza kufanya kazi ‘babkubwa’ Zoo na zikachezwa kwenye vituo vya redio vya kijanja.
Studio hiyo inakwenda kwa jina la ATP na inapatikana pande barabara ya Rufiji jijini humo, na Meneja wa Studio hiyo, Iku Mwakisambwe, alisema nasi kwamba lengo ni kupandisha kiwango cha wasanii wa Rocky City ili kikubalike kimataifa.
Mastaa ambao tayari wameingiza voko kwenye studio hiyo ni Dark Master, Geez Mabovu, Z- Anto, Bwana Misosi, Chelea Man na wengine. Hey, Jitaman, H. Baba, Fid Q, Hard Mad, Rado na wengine, mnaweza kufikiria kurudi nyumbani?
**************************
JenniferLove
Aanza ngono akiwa na miaka 14, ametoa uroda kwa njemba 24
Ebwana Dah! Staa wa muvi, Jennifer Love Hewitt ndiye anaye take cover kwenye safu hii na hapa inatajwa orodha ya njemba ambazo kwa nyakati tofauti amezikabidhi penzi lake.
Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti inayodili na ishuz za uhusiano wa mastaa wa mbele kwenye eneo la nani kamrukia nani, Jennifer Love alianza kuchangamkia sanaa ya kitandani akiwa na umri miaka 14 tu. (Aliwahi sana).
Scott Bairstow ndiye kidume anayetajwa kuanza kuchangamka naye mwaka 1994 ambapo Jennifer alikuwa na umri wa miaka 14. Akaja Joey Lawrence ambaye alichangamsha damu kwa mwaka mmoja, 1995 – 96, akiwa na miaka 15.
Alipotoka kwa Joey, Jennifer kwa mtindo wa bandika bandua, alijiweka kwa Will Friedle ambapo penzi lao lilidumu kuanzia mwaka 1996 – 97 kabla kuamua kuutua mwili wake kwa Andrew Keegan, 1997.
Penzi la Jennifer na Andrew lilidumu kwa muda mfupi mno na baada ya kutoka kwake alihamishia majeshi kwa Carson Daly kuanzia mwaka 1997 – 99.
Hata hivyo, akiwa na Carson, Jennifer ‘alichiti’ na kumgea kidogo Jeff Timmons mwaka 1998. Mwaka 1999 alijipumzisha kwa muda kwa Diego Serrano kabla ya mwaka huo huo kutuliza mizuka kwa Rich Cronin ambaye alikaa naye mpaka mwaka 2001.
Kwa mara nyingine, Jennifer akiwa na Rich, mwaka 1999 ‘alimchiti’ na kumegana kisela na Wilmer Valderrama, pia mwaka 2000 kwa Alec Baldwin.
Aidha, mwaka 2000 huo huo, alianzisha uhusiano na Craig Bierko na kudumua naye mpaka mwaka 2001. Hii inamaana kuwa mbali na ‘kuchiti’ mara kwa mara kwa watu tofauti, pia kati ya kipindi cha mwaka 2000-01, Jennifer alikuwa na wanaume wawili permanent, Craig na Rich.
Mwaka 2001-02, Jennifer alijiweka kwa Patrick Wilson, pia mwaka 2001, hakuona soo kumpa penzi lake Enrique Iglesias, mwaka 2002, alimegana na Shaggy, mwaka huo huo akajikunja na John Mayer, na kuanzia mwaka 2002-03, alimchagua Paul Nicholls. Baada ya hapo, Jennifer akajiweka kwa John Cusack, hiyo ilikuwa ni mwaka 2003, mwaka huo huo akajikunja na Stephen Dorff, Kip Pardue, Antonio Sabato na Scott Austin ambaye walimwagana mwaka 2004.
Mwaka 2004, alijiweka kwa Will Estes, mwaka uliofuata, hapo unazungumziwa 2005, alikaa kwa Ross McCall ambaye walitosana mwaka 2009 na baada ya hapo akahamia kwa Jamie Kennedy ambaye yupo naye mpaka sasa.
Jennifer, alizaliwa Februari 21, 1979, Waco, Texas, Marekani, kwahiyo ana umri wa miaka 30.
*******************************************
compiled by mc george
for more news visit: www.globalpublisherstz.com

No comments:
Post a Comment