Tuesday, June 29, 2010

Unajua kwanini tunaugua mara kwa mara? - 5

Tunawaletea mfululizo wa makala haya yenye lengo la kujua sababu za watu kuugua mara kwa mara. Tumeanza kwa kuona kuwa mwili una kanuni zake ambazo ni lazima zifuatwe na zisipofuatwa huleta maradhi. Vile vile tumeona kuwa maradhi hayaji ghafla, bali huanza kwa kutoa ishara ambazo watu wengi, ama hawazijui au huzipuuzia, tunahitaji kuwa na elimu ya kutosha kuhusu ulaji wa vyakula vya aina mbalimbali…Sasa endelea.

Maziwa bora ni yale yaliyoondolewa mafuta au krimu yake yote na kubaki na virutubisho pekee (Fat Free).

Kwa mantiki hiyo, unaponunua maziwa, nunua maziwa yaliyoandikwa Fat Free au Low Fat badala ya kununua yale yaliyoandikwa Full Cream ambayo huwa na mafuta mengi yanayaoweza kukusababishia matatizo ya moyo au shinikizo la damu.

Aidha, iwapo unakamua au kutayarisha mwenyewe maziwa halisi ya ngo’mbe, unashauriwa kuyachemsha kwanza kisha uyaweke yapowe na baada ya hapo engua ule utandu wa juu (malai) na kuuweka pembeni, kwani hayo huwa ni mafuta ambayo siyo mazuri kiafya.

Najua kwamba, kama kuna kitu ambacho kinapendwa sana na watu kwenye maziwa, basi ni pamoja na huo utandu na kuna watu wengine hula utandu pekee na kuacha maziwa yote. Kwa ladha ni matamu sana, lakini kwa kuyala kwa muda mrefu ni hatari kwa afya yako.

Mayai
Ulaji wa mayai nao unahitaji tahadhari. Yai ni miongoni mwa vyakula muhimu kwa afya ya binadamu na vinavyopendwa na watu wa rika mbalimbali. Yai nalo linatakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo na kwa kuchagua, kwani siyo lote ni zuri kiafya.

Tunapokula yai, tunashauriwa kuepuka kula kiini chake na badala yake kula sehemu nyingine ya yai. Kiini cha yai siyo kizuri kiafya, kwa namna moja au nyingine huchangia matatizo ya moyo na shinikizo la damu, iwapo yataliwa kupita kiasi. Mtu mwenye matatizo ya presha au moyo, hatakiwa kula mayai kabisa.

Samaki
Chakula kilichopo katika kundi hili ambacho ni salama zaidi ni samaki na nyama za aina hiyo, wakiwemo kuku. Nyama ya samaki pamoja na mafuta yake, yameelezwa kutokuwa na madhara kwa afya ya binadamu, hivyo ulaji wake ni salama zaidi kuliko aina nyingine za nyama. Mlaji hujipatia kinga ya magonjwa ya moyo anapokula samaki.

Kwa kula nyama ya samaki unapata protini iliyo safi mwilini lakini pia mafuta yake ni dawa ya magonjwa ya moyo, hata dawa za Omega 3, zimetengenezwa kutokana na mafuta ya samaki ambayo yameonekana kutokuwa na madhara kwa binadamu.

Kuku
Nyama ya kuku kwa ujumla wake ni nzuri na salama kiafya, ila kuku ana tofauti kidogo na samaki, kwa sababu kuna sehemu zingine za nyama ya kuku siyo salama kutokana na kuwa na mrundikano mwingi wa mafuta. Unapokula nyama ya kuku, epuka kula pamoja na ngozi yake.

Chuna ngozi, ikiwezekana kuku mzima na kisha kula nyama yake nyeupe isiyo na mafuta na epuka kula vitu kama firigisi na nyama ya mgongo, kwani sehemu hizo huwa na mafuta mengi sana ambayo siyo mazuri kuliwa.

Itaendelea wiki ijayo...

4 comments:

Unknown said...

tunashukuru kwa darasa lako zuru,
samahani naomba kuuliza.
mimi napenda sana nikipika dagaa wa kigoma, mwisho kabisa nawawekea cream ya maziwa badala ya nazi ambayo ninakuwa nimeitenga kutoka katika maziwa fresh, je hii pia ina madhara mwilini?

ni kweli cream ni mbaya kwa afya, kwani mimi huitenga na kutengeneza samli baadaye,
je hii samli itokanayo na cream hiyo pia ina madhara mwilini?

asante sana

Mrisho's Photography said...

BAZIZANE: CREAM ya maziwa inayotolewa kwenye maziwa kabla ya kupikwa tena siyo nzuri kwani kuna kiasi kikubwa cha mafuta mabaya..hivyo unashauriwa kutopenda kuitumia sana.

ila cream hiyo ukitengeneza SAMLI (GHEE AU CLARIFIED BUTTER) Inakuwa haina madhara badala yake ina faida mwilini, kwani mafuta mabaya yote yanakuwa yametoka...soma maelezo haya kwa uelewa zaidi:

Why is ghee so healthy?

Ghee’s chemistry holds the secret to its health benefits. Humans need both saturated and unsaturated fats as part of a healthy diet. Ghee is made from a combination of saturated and unsaturated fats. It is about 65% saturated fat and 25% monounsaturated fat with about 5% polyunsaturated fat content. Its saturated fat is primarily (89%) made from the easy-to-digest short chain fatty acids and it contains 3% linoleic acid which has anti-oxidant properties. It also contains the fat soluble vitamins Vitamin A, D, E and K.

It has been suggested that ghee actually benefits the HDL:LDL ratio. One study has even shown that ghee can lower high cholesterol. As part of a lacto-vegetarian diet ghee offers important nutritive benefits. As a healthy oil ghee can help replace oxidised fats populating cell membranes and help the body in maintaining a low state of oxidation.

Unknown said...

Kaka Mrisho may Allah bless you always.

PAM said...

SASA MI MBONA SIKU ZOTE NAAMBIWA KIINI NDO CHENYE AFYA NA SI SEHEMU NYINGINE YA YAI NA NDO MAANA TUNAAMBIWA HATA MTOTO KWENYE UJI WAKE IKIWEZEKANA UCHANGANYE NA KIINI CHA YAI BICHI LA KIOENYEJI?