Monday, July 12, 2010

FFU wa Ngoma Africa Band Kutumbuiza pia AFRILU FESTIVAL


FFU wa Ngoma Africa Band kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa la AFRILU Festival,mjini Ludwigshaven, siku 24 -07-2010 Jumamosi ambako washabiki wa mziki na wakazi wa miji ya Manheim na Heidberg,Ujerumani watajipendelea kwa kucheza mziki wa bendi hiyo maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" ambayo ina mazoea ya kuwatia kiwewe washabiki wa mziki kila wanapotumbuiza.
bendi hiyo iliyoanzishwa 1993 na kufanikiwa kujizolea washabiki kila kona duniani,imejikuta na kazi ngumu ya kuwapa burudani washabiki wake ambao ndio ma boss wa bendi bila ya kumpuzika!
Ngoma Africa band kwa sasa wanawasha moto wa kimataifa na singo CD mpya "Jakaya Kikwete 2010"
unaweza kujipa raha kwa kusikiliza nyimbo at www.myspace.com/thengomaafrica pia jumuika nao katika baraza la
www.facebook.com/ngomaafrica wasiliana nao ngoma4u@googlemail.com

1 comment:

Anonymous said...

ngoma africa band wakubwa wa mambo! mziki wenu mkubwa tena umeenda shule.