Monday, August 30, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Hakuna ngono Millosis – Mr. Chuz
Mkurugenzi wa Kundi la Fukuto Arts Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’, amesema ndani ya tamthiliya mpya anayoiandaa iitwayo Millosis ambayo itarushwa na kituo kimoja cha runinga hivi karibuni, hakuna vitendo vya ngono.

Akiteta na kona hii, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Chuz alisema, ingawa tamthiliya hiyo itaendeshwa kwa mtindo wa Big Brother, lakini hakutakuwa na maonesho ya mambo yoyote yanayoashiria vitendo vya ngono.

“Nimeanza kupata chalenge kutoka kwa watu mbalimbali, kwa sababu mchezo mzima utakuwa katika Jumba la Millosis basi wanadhani kwamba kutakuwa na mambo machafu. Hapana...hizo ni fikra potofu... Ni tamthiliya iliyolenga kujifunza na kuelimisha zaidi. Inakidhi kuangaliwa na watu wa rika zote,” – Chuz.
*****************************

Kat DeLuna Afungua pazia la wanaume na Omarion!
Ebwana Dah wiki hii inarudi tena kwa mwanamuziki wa mbele, Kat DeLuna ambapo kwa mara ya kwanza inafahamika kwamba anaanguka kitandani na Omarion Grandberry.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 22, aliyezaliwa Novemba 17, pamoja na umri alionao grafu ya wanaume wake ndiyo kwanza imenaswa mtandaoni kwa mara ya kwanza.

Awali, safu hii iliwahi kuripoti kwamba, mwanamuziki huyo hajawahi kupata kashfa ya kulala na mwanaume kitanda kimoja, lakini sasa safari ndiyo imeenza! Dah!
***********************************

JI ampiga bao Ray C kenya
Guy aliyefanikiwa kuiteka Bongo Flava kwa songi moja, Juma Issa ‘JI’ amempiga bao Kiuno Bila Mfupa, Rehema Chalamila ‘Ray C’ na kwa sasa dogo yupo kwenye tour ndefu kwenye himaya ya Kibaki yenye Katiba Mpya, Kenya.

JI a.k.a J-Inshu amepewa ulaji huo kupitia mradi wa Maliza Umaskini na tour hiyo ilikuwa itekelezwe na Ray C kabla ya wahusika kutengua makubaliano. Kwa mujibu wa CEO wa Maliza Umaskini, Sadat Muhindi, JI atafanya ziara zote ambazo zilikuwa zitekelezwe na Ray C.


Sadat, aliiambia Abby Cool & MC George over the weekend Ijumaa iliyopita kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kwenye Facebook kuwa lengo la ziara hizo ni kuutangaza mradi wa Maliza Umaskini, kulipa promo kundi chipukizi la MU Family.

Alisema: “Pia ni kumkuza JI, leo (Ijumaa) atafanya shoo Mumias Town kwenye Ukumbi wa Westgate, kesho (Jumamosi) atakamua kwenye Ukumbi Pinewood, Kitale na Jumamosi inayokuja atakuwa Poa Place, Eldoret town na siku inayofuata atafunika katika Ukumbi wa Matunda Primary, Lugari.” Hivi karibuni, Ray C aliingia kwenye mgogoro na Sadat ambaye alikatisha makubaliano ambayo walikuwa wameingia awali ya kufanya ziara za mradi wa Maliza Umaskini nchini Kenya.

Ray C alilalamika kulazimishwa ngono lakini Sadat aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kwamba madai hayo si ya kweli kwa sababu mwanamuziki huyo alionesha utovu wa nidhamu ndiyo maana wakamuengua kwenye Maliza Umaskini ambao ni mradi wenye kusimamia maadili katika kupambana na matatizo ya kiuchumi hasa kwa vijana.
*********************************************************************

K-sher Stop Tip Top
First Lady wa Kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake pande za Manzese, Dar es Salaam, Khadija Shaban a.k.a K-Sher amesimamishwa kupiga mzigo ndani ya kundi hilo kwa kipindi kisichojulikana.

Akidondosha stori ndani ya ShowBiz wikiendi iliyopita Meneja wa kundi hilo, Khamis Tale Tale a.k.a Babu Tale alisema kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya K-Sher kuonesha utovu wa nidhamu kitu ambacho kimekuwa kikiwapa usumbufu kwa muda mrefu.

“Mara nyingi K-Sher amekuwa akifanya vitu ambavyo vinaleta usumbufu kwa wenzie, mfano hivi karibuni tulikuwa na shoo Mwanza, yeye alishindwa kufika kwa sababu tulishindwa kupata tiketi ya ndege kwa muda huo, wenzie walikuja kwa basi na kufanya shoo kisha kurudi Dar.

“Tulipofika Dar akawa anadai alipwe pesa za shoo hiyo, huku akitishia kujitoa kundini kama hatukufanya hivyo, siyo hilo tu yapo mengi ambayo msanii huyo amekuwa akiyafanya na kusababisha usumbufu kwa wenzie kitu ambacho kimetusukuma sisi viongozi kuchukua uamuzi wa kumsimamisha mpaka hapo baadaye,” alisema Tale.

Safu hii ilijaribu kumtafuta K-Sher kupitia simu yake ya mkononi ili naye aweke wazi kuhusu hilo lakini mpaka tunakwenda mitamboni hakuweza kupatikana. Tunaahidi tutaendelea kucheki naye, atakapopatikana kila kitu kitakuwa wazi kupitia gazeti ndugu na hili, Ijumaa litokalo kila siku ya Ijumaa. ***************************************

Tanzanite aokolewa na mabaunsa
Msanii chipukizi ndani ya game ya Bongo Fleva anayekwenda kwa jina la Mwingereza Athumani a.k.a Tanzanite ilikuwa kidogo mambo yamwendee vibaya aliponusurika kudondoka jukwaani baada ya juhudi za mabaunsa kuwa za ukweli, Hemed Kisanda anaandika.

Mtiti huo ulichukua nafasi pande za Tanga, alipokuwa mkoani humo kugonga shoo, lakini akiwa jukwaani aliishiwa nguvu na kutaka kudondoka kabla ya mabaunsa kuonesha kwamba wanajua kazi yao vyema. Tanzanite alipovutiwa waya na kona hii alisema:

“Ni kweli niliishiwa nguvu katikati ya shoo, nilikuwa mgonjwa, ila sikutaka kuwaboa mashabiki wangu wa Tanga, lakini namshukuru Mungu niliwahishwa hospitalini na kwasasa nipo poa.”
****************************

Lulu anahitaji kushauriwa – Dk Cheni
Kichwa cha ukweli ndani ya Kiwanda cha Filamu Bongo, Mahsein Awadh, ameibuka kwa mara nyingine ndani ya mjengo wa ShowBiz , safari hii akimwaga machozi yake kwa msanii ‘kinda’ katika field hiyo Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisema kwamba anatakiwa kushauriwa. Mwana-ShowBiz Jelard Lucas anashusha mzigo.

Akiongea na kona hii wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Dk. Cheni alisema, anaumizwa sana na vitendo vinavyoripotiwa magazetini juu ya msanii huyo kwakuwa haviendani na yeye.

“Naumia mara mbili, kwanza mimi ndiye niliyempeleka Kaole, kwahiyo naumia kama mgunduzi wa kipaji chake, lakini pia naumia kama msanii mwenzake na kaka yake. Unajua kinachoonekana ni kwamba Lulu hajapata mshauri, anatakiwa kushauriwa, hasa na dada zake,” alisema Dk. Cheni kwa masikitiko. *******************************************


Compiled by MC George/Wikienda

1 comment:

emu-three said...

Ahsante kwa madondoo hayo