Sunday, October 31, 2010

BOTSWANA YAITOA AFRIKA KIMASOMASO MISS WORLD

Miss Botswana 2010 Emma Wareus
Miss United States, Alexandria Mills, ndiye Mrembo wa dunia baada ya kuwagaragaza wenzake 100 wakati wa fainali hizo zilizofikia tamati usiku wa kuamkia leo katika mji wa maraha wa Sanya, nchini China. Mrembo huyo, bado binti mbichiii kwani ana umri wa miaka 18 tu! kwa upande mwingine Mrembo wa Botwasana, bibie Emma Wareus ameitoa Afrika kimasomaso baada ya kushika nafasi ya pili mbele ya mrembo wa Venezuela, Adriana Vasini. Tunaambiwa kwamba mrembo wetu wa Tanzania hata 50 bora hakukanyaga!!!

No comments: