Tuesday, November 23, 2010

ASALI: KIBOKO YA UNENE UNAOWAKERA WANAWAKE-2

Karibuni tena katika sehemu ya pili ya makala yetu ya leo kuhusu kupunguza unene, mada ambayo imeonekana kuvuta hisia za wasomaji wengi. Tatizo la unene limekuwa sugu. Kila mmoja anajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hilo.

Wiki iliyopita nilianza kuelezea uzito anaopaswa kuwa nao mtu kulingana na urefu wake. Kwa kuzingatia maelezo yale, sina shaka sasa umeshajua unatakiwa kupunguza kilo ngapi.

Ingawa kuna baadhi ya wasomaji wametaka kujua jinsi ya kuongeza uzito, lakini kwa leo hatutaweza kuzungumzia hilo, tutaandaa makala yake siku nyingine, kwa sababu ni vitu viwili ambavyo vinahitaji kuongelewa kwa upana.
KANUNI ZA KUPUNGUZA UZITO
Kanuni ya kwanza ya kupunguza uzito inatueleza kuwa ili mtu upunguze uzito, unahitaji kutoa kalori nyingi mwilini na kuingiza kalori kidogo (Less Calories In + More Calories Out= Weight Loss). Kwa lugha nyepesi, unapokula chakula chochote unaingiza kalori mwilini na unapofanya mazoezi au kazi yoyote unatoa kalori mwilini.

Hivyo kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako.
ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE
Baada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula.

Matumizi ya asali ni rahisi sana. Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya.

Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali.

Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya ‘fructose’ (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.

Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki.

Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.

ASALI NA MDALASINI
Mchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya asali, abdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku.

Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa adbalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha asali (saizi ya kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka.

Anza kuchanganya maji moto na unga wa abdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.

Itaendelea wiki ijayo...

7 comments:

Anonymous said...

"Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina."

Ushauri sahihi. Ni lazima kufanya diet na kufanya mazoezi. Asiye mtu anayeshinda baa akila nyama choma na kurudi nyumbani kulala akasema kwamba atakula asali tu na atapunguza unene. KULA CHAKULA KIDOGO CHENYE AFYA + MAZOEZI and then hii asali.

Mwisho: Jenga tabia ya kutoa link ambako watu wadadisi kama mimi tunaweza kusoma haya maoni au tafiti hizi. Naona hata mzozo wa kwanza kuhusu hii topic ulizuka baada ya yule Dr (a.k.a mbeba maboksi wa Houston Texas) kudai source ya hizi info unazoweka hapa. Nadhani hili ni jambo la msingi na usilipuuze. Weka link ili watu wakajisomee zaidi huko.

Otherwise, good job kwa kujaribu kusaidia.

Finally: wewe ndiye Mkurugenzi msaidizi wa Global Publishers au nimechanganya mambo?

Mkosamali said...

Kaka Mrisho ebu nambie tiba hii na kwale wazeia wa kinywaji,itafanya kazi kweli??

Mrisho's Photography said...

..ushauri wako wa kuweka link kwa humu nimeuzingatia, nitakuwa nikifanya hivyo matoleo yajayo au wakati namaliza mada hii...kwani ili kuwa na information za kutosha, ni lazima upate taarifa kutoka sources mbalimbali na siyo moja tu..hivyo zitakuwepo link kadhaa na mtaweza kujisomea kwa undani zaidi kwa wakati wenu.....kuhsu mimi...siyo Mkurugenzi Msaidizi..umechanganya mambo...asanteni.

Anonymous said...

hongera kwa moyo wako wa kuwasaidia watu wanene kama sisi kupungua bt mm nna maswali kadhaa naomba unijibu.kwanza itamchukua mtu mda gani mpaka mtu aweze kupunguza kilo 13 kwa kutumia hiyo tiba yako?pili ni kwamba mtu akishapunguwa kilo anazotaka hiyo asali aiache au ndo ainywe maisha yake yote ili asinenepe tena?na pia hiyo tiba ina usalama kwa afya ya mtu kwa asilimia ngapi?ni hayo tu ntashkuru sana kama utanijibu maswali yangu kwa haraka,kazi njema

Mrisho's Photography said...

utapunguza kilo 13 kwa siku ngapi inategemea na wewe mwenywe utatumia vp asali hiyo, utafanya mazoezi kiasi gani na utafuata masharti mengiine kiasi gani...hakuna jibu la moja kwa moja..inategemea mwenyewe.

ukimakamilisha lengo lako unatakiwa kuacha kutumia. Kutokunenepa kutategemea na wewe mwenywe utaendelea na staili ipi ya maisha...you are what u eat..!

tunachoandika hakina sha na siyo kigeni, wataalamu walishafanya utafiti kabla mimi na wewe hatujazaliwa...still u can do ur own research....just google: Honey and cinnamon.....

Unknown said...

And you are what you digest also

Unknown said...

And you are what you digest also