Mbunge wa Jimbo la Liwale Bi. Faith Mitambo (wa pili kulia), akimsaidia mtoto
Fadhila Lupepa, ambaye ni mlemavu wa viungo, baada ya kumkabidhi msaada wa
baiskeli jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Paul Chiwile na Mama wa mtoto
huyo Esha Nokota.
Fadhila Lupepa, ambaye ni mlemavu wa viungo, baada ya kumkabidhi msaada wa
baiskeli jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Paul Chiwile na Mama wa mtoto
huyo Esha Nokota.
Mbunge wa Jimbo la Liwale Faith Mitambo (wa pili kushoto), akikabidhi seti ya
jezi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Serengeti FC, Johnson Raymond (kulia, wakati wa hafra ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo iliyofanyika mjini Liwale jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Chiwile.
jezi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Serengeti FC, Johnson Raymond (kulia, wakati wa hafra ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo iliyofanyika mjini Liwale jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Chiwile.
Mbunge wa Jimbo la Liwale Bi. Faith Mitambo (kulia) na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw.
Paul Chiwile, wakishiriki kusukuma baiskeli maalum za watu wenye walemavu, baada ya kuwakabidhi mjini Liwale jana.
Na Mwandishi Wetu, LiwalePaul Chiwile, wakishiriki kusukuma baiskeli maalum za watu wenye walemavu, baada ya kuwakabidhi mjini Liwale jana.
WANANCHI wa Jimbo la Liwale, mkoani Lindi, wameaswa kuvunja makundi na
kuunganisha nguvu zao pamoja ili waweze kuijenga upya wilaya yao. Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Liwale kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Faith Mitambo, wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
Bi. Mitambo amesema kazi kubwa ya mbunge ni kushirikiana na wananchi kuhakikisha maendeleo ya kweli yanapatikana, hivyo akawaasa kuwa iwapo watashirikiana nae vizuri katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake mabadiliko yataonekana.
"Ndugu zangu wana Liwale, kipindi cha misukosuko ya uchaguzi kimeisha, mbunge wa
jimbo letu amepatikana, ambaye ni mimi Faith Mitambo, kazi yangu ni kushirikiana
nanyi kuleta mabadiliko," amesema Bi. Mitambo.
Amewaambia wananchi kuwa miaka mitano ya uongozi wake, anakabiliwa na changamoto nyingi, ambazo iwapo atapata ushirikiana mzuri kutoka kwa wananchi na watendaji wa halmashauri, kwa pamoja watafanikiwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Bw. Paul Chiwile, alimwambia Bi. Mitambo kuwa
baada ya wabunge kuapishwa mjini Dodoma, wananchi walilipuka kwa furaha, jambo
ambalo lilionesha kuwa na imani naye.
Mkuu huyo wa wilaya alisema alipofika Liwale kama Mkuu wa Wilaya mwaka 2009,
hapakuwa na mawasiliano kati yake na mbunge, jambo ambalo ni mzigo katika
kuendesha Serikali.
"Sikuwa na mawasiliano na mbunge aliyepita, hakukuwa na utaratibu wa kuonana
wala kubadilishana mawazo, nilifanya kazi kwa wakati mgumu sana, kuchaguliwa kwa Bi. Mitambo na kuapishwa kumenipa faraja sana," alisema.
Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Liwale, Bw. Mohamed Ngomambo, amesema jimbo hilo limepata kiongozi imara katika ngazi ya ubunge na kuwaasa wananchi kumtumia
vizuri ili kuharakisha maendeleo.
Katika ziara hiyo, Bi. Mitambo alikabidhi msaada wa darubini mbili zenye thamani
ya sh. milioni 3 kwa Hospitali ya Wilaya ya Liwale na baiskeli tano za kubeba
wagongwa, baiskeli 45 za walemavu wa viungo, kompyuta moja kwa CCM na sh.
milioni 1 kwa mtandao wa akinamama wajasiriamali (WAMALI).
(stori picha na Willy Edward)
No comments:
Post a Comment