Monday, May 30, 2011

Rota ndiye kinara wa Serengeti Fiesta Free Style 2011 ndani ya Morogoro

Ni kijana wa makamo hivi ambaye alionyesha kipaji cha kufreestyle kwa kiwango cha juu kabisa, anaitwa Rota Flavian Komba ndiye aliyeibuka kinara wa msimu wa dhahabu wa unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 ndani ya mji wa Morogoro jana jioni. Kufuatia ushindi huo Rotas atakwenda jijini Dar kupambana na vinara wengine kutoka mikoa mingine katika mpango mzima wa kutimiza kilele cha msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta 2011 ndani ya jiji la Dar,itakayofanyika hapo baadaye.
Pichani kulia ni Rota akishusha mistari yake katika mtindo huru mbele ya hasimu wake Hanstar,katika mtindo ule wa Kubato,wakiwa katika hatua ya mwisho a.k.a fainali,kwamba atakayeshinda ndiye kinara wa msimu wa dhahabu wa unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 ndani ya mji wa Morogoro.
Pichani ni Washiriki Wanne kati ya washiriki 44 walioingia nusu fainali katika suala zima la kumsaka mkali wa msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,kutoka kulia ni Rotas,Slim,Ras Q pamoja na Hanstar.
Baadhi ya wakazi wa Morogoro wakifuatilia shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011 jioni ya leo ndani ya ukumbi wa club ya Four Stars,mjini Morogro.
Pichani ni Vijana wa Morogoro,kushoto ni Goligota pamoja na Ras Q wakionesha umahiri wao wa kubato katika mtindo huru.
Majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011, Zavara pamoja na Skwiza wakijadiliana jambo.
Mratibu wa Serengeti Fiesta Free style, ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 ya jijini Dar, Ruben Ndege akitaja washiriki walioingia kwenye hatua ya 16,ambapo pia mchuano ulifanyika na kuwapata washiriki nane ambao walifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,ndani ya mji wa Morogoro.
Mwanadada akiamsha hamasa kwenye shindano la Fiesta Freestyle 2011.
Mmoja wa washiriki aitwaye Abhou akionyesha uwezo wake wa kughani mbele ya mashabiki kibao .
Mwanadada mwingine aitwaye Khadija nae akionesha umahiri wake wa kushuka mitindo hur.
Mratibu wa Serengeti Fiesta Freestyle, ambaye ni mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar akieleza utaratibu mzima kwa washiriki.
Pichani majaji wa shindano la Serengeti fiesta freestyle 2011,wakifuatilia kwa makini namna washiriki wanavyoonyesha vipaji vyao vya kughani.

Kwa pamoja wakilianzisha.
Jaji wa shindano la Serengeti fiesta freestyle 20011 ndani ya mji wa Morogoro,Chief Rhamson a.k.a Zavara akifafanua jambo kwa Dj Fetty kabla ya mchakat.
Washiriki wakiratibiwa vyema bin sawia ile shindano lienze.

Baadhi wapenzi na washabiki wa mitindo huru wakifuatilia kwa makini shindano hilo linalovuta hisia za vijana wengi.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakiwa wamejitokeza jioni ya leo kwenye shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,linalofanyika ndani ya ukumbi wa Club ya Four Stars,Mjini Morogoro.

No comments: