Wednesday, October 19, 2011

Daktari Mtanzania Julie Makani apokea tuzo kutoka Royal society Pfizer London

Dr Julie Makani.(kushoto) akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo. JPG
Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr  Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba
Bob Makani (kushoto) akiwa na binti yake
 Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake
Salam,            
 Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo  jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr  Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kukuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)

 Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya  Anaemia kwenye  ugonjwa Sickle Cell

Ni matumaini yake  kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya  na jamii kwa ujumla.
Kwa niaba ya Watanzania  wote  Urban Pulse tunapenda kumpongeza  DR Makani kwa mafanikio hayo.

Asanteni

Urban Pulse Creative

No comments: