Thursday, October 20, 2011

UN YAKARABATI MADARASA MAWILI SHULE YA MSINGI TANDALE

Diwani wa Kata ya Tandale Jumanne Amiri  Mbunju akishukuru shirika hilo kwa kuichagua shule ya Msingi Tandale kwa kuifanyia ukarabati wa madarasa mawili ambapo pia ameliomba shirika hilo kuikumbuka shule hiyo tena mwakani  wakati wa maadhimisho kama hayo. Diwani Mbunju pia ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi kushiriki katika kutoa michango ya kuboresha mazingira ya kata ya Tandale.
Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Hassani Kalinga (wa pili kushoto) akimkaribisha Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen (wa pili kulia). Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandale Renatus Pallu na Kulia ni Diwani wa Kata ya Tandale Jumanne Mbunju.
"Kwa herini watoto wazuri UN inawapenda na inawajali": Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akigana na wanafunzi wa shule ya Msingi Tandale.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandale.
Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen akionyesha mfano kwa vitendo wakati wa shughuli za ukarabati wa madarasa hayo.
 
unaweka Urembo pembeni tunapiga kazi: Hoyce Temu naye alishiriki.
Baadhi ya Walimu wa Shule ya msingi Tandale.

No comments: