Mwendeshaji wa kipindi
cha Njia Panda kinachorushwa na redio ya Clouds FM,Dr Isaac Maro (kulia)
akiutazama mguu wa Mzee Rasmo Kilata ambaye mguu wake ulikatwa mara
baada ya kuathiriwa na ugonjwa kansa,ambao ulitokana na kidonda chake
alichokipata kwa muda mrefu bila kupona,Mzee huyo wa makamo mwenye
watoto 3 na wajukuu wasio na idadi pia ni mlemavu wa ugonjwa
ukoma,Shoto ni Mwenyekiti wa Kampeni ya Tanzania Gives Back,Edmond
Lyatuu akiwa pamoja na mratibu wa Kampeni hiyo,Dada Susan,kampeni hiyo
ya Tanzania Gives Back 2011 inaratibiwa na kituo cha Tanzania House Of
Talent (THT).
Mwenyekiti wa kampeni ya Tanzania Gives Back 2011,Edmond Lyatuu
pichani kulia akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi mapema
leo asubuhi kwa baadhi ya wazee waishio kwenye kambi ya Walemavu na
Wasiojiweza ya Nunge,Vijibweni-Kigamboni jijini Dar es salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ditto
akiimba moja ya wimbo wa kuwafariji na kutia moyo wazee hao ambao
wengi wao wameathiriwa na ugonjwa wa ukoma.Wazee hao wanaishi kwenye
kijiji hicho cha Nunge chenye jumla ya nyumba 50,ikiwa na idadi ya
familia 72,ambapo kila nyumba inakaliwa na watu 5 mpaka 7.Akizungumza
kwa niaba ya wenzake Mzee Issa Ally ameiomba Serikali na wadau wengine
kuja kuzikabarabati nyumba zao wanazoishi kwani kwa sasa zimechakaa
sana,amesema na kuongeza kuwa wanahitaji msaada mkubwa wa kupuliziwa
dawa ya kuuwa wadudu katika nyumba zao,kwani kumekuwepo na wadudu
wengi wakiwemo Viroboto,Mende na wengineo ambao wamekuwa wakiwapa
taabu sana.
Wanaharakati wa kampeni ya Tanzania Gives Back wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wazee hao.
Mwenyekiti wa Tanzania Gives
Back,Edmond Lyatuu akizungumza na baadhi ya wazee wenye ulemavu wa
mikono,macho na miguu kutokana na kuathiriwa na ugonjwa wa Ukoma,Wazee
hao wametoa kilio chao kwa Serikali na wadau mbalimbali kwamba
wajitokeze kuwasaidia wazee wao kwa namna moja ama nyingine,kwani kwa
sasa wamekuwa wakiishi katika hali ngumu hivyo bado wanahitaji msaada
mkubwa wa hali na mali.
Mwanaharakati,Mama Sadaka Gandi kutoka
THT,ambao ndiyo waratibu wa kampeni ya Tanzania Gives Back,akizungumza
na Wazee waliothiriwa na ugonjwa wa Ukoma mapema leo asubuhi kwenye
kambi yao ya Nunge ilioko Vijibweni-Kigamboni jijini Dar es
salaam.
Dada Kemi kutoka Tanzania Gives back
akiongea na kuwafariji Wazee walioathiriwa na ugonjwa wa Ukoma,Wazee
hao ambao wamekuwa wakiishi kwenye kijiji hicho kilichoanzishwa rasmi
mnamo mwaka 1975 na kuanza kuhudumiwa na Serikali,wamewashukuru sana
wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakitokeza na kuwapa misaada
mbalimbali ambayo imekuwa ikiwasaidia kwa kikubwa,ingawaje wanakiri
kuwa bado haitoshi hasa kulingana na mahitaji yao ya kila
siku.
Pichani na juu ni wazee wakiwasikiliza wageni wao waliofika
kuwatembelea mapema leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Tanzania Gives Back
2011,Edmond Lyatuu akizungumza na Afisa Kilimo Msaidizi wa kituo hicho
cha Walemavu na wasiojiweza kiitwacho Nunge, Bwa. Frank Mnuo mambo
mbalimbali yahusuyo kituo hicho pamoja na changamoto
wanazozipata.Shoto ni Dada kemi ambaye pia ni mmoja wa waratibu wa
kampeni hiyo.
No comments:
Post a Comment