Na Mwandishi wetu.
Siku chache zilizopita yamefanyika maonesho ya mitindo ya
mavazi ya Swahili Fashion Week nchini Angola (Fashion Business) yaliyobuniwa na
mbunifu wa mavazi kutoka Tanzania almaarufu kama Mustafa Hassanali.
Tarehe 22 Oktober 2011 yanafanyika maonyesho ya mavazi
nchini Afrika Kusini chini ya udhamini wa kampuni ya Precision Air yanayotambulika
kwa jina la AFI Africa Fashion week ambapo Tanzania inawakilishwa na mbunifu
Mustafa Hassanali.
Ufafanuzi tunaotaka kuutoa hapa ni kwamba inajulikana kuwa
katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kwa mara ya kwanza mbunifu huyo atazindua
chata ya ‘UHURU’ambayo inawakilisha Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961.
Kwa uhakika sio mara ya kwanza kuzinduliwa kwa ‘UHURU
Collection’ kumefanywa na mbunifu huyo na katika kuwawekeni wazi chata ya ‘UHURU’
inamilikiwa na Wabunifu Mahiri wa Mavazi VIDA MAHIMBO na ALLY REMTULLA.
Wakizungumzia chata ya ‘UHURU COLLECTION’ wabunifu hao
wamesema kuwa kwa mara ya kwanza chata hii ilizinduliwa mwezi February 2011
visiwani Zanzibar.
Nembo hii imesajiliwa na inamilikiwa na VIDA MAHIMBO na ALLY
REHMTULLAH chini ya Karisma Fashion Group Limited na ndio maana wakati wa
uzinduzi ilijulikana kwa jina la UHURU The African Freedom by ALLY REHMTULLAH
na VIDA MAHIMBO, for the young and the old, the daring & the conservative…It’s
a brand for us all.
Sio kweli kwamba ‘UHURU COLLECTION’ imebuniwa na Mustafa
Hassanali na sio kweli kwamba inazinduliwa mara ya kwanza.
Kwa ufafanuzi huu unapohitaji bidhaa yoyote ya ‘UHURU
COLLECTION’ wasiliana na VIDA MAHIMBO au ALLY REHMTULLAH @ duka lake la Slipway Shopping Centre-VIDA
MAHIMBO STORE.
Tembelea mtandao www.freeuhuru.com
No comments:
Post a Comment