Saturday, October 22, 2011

WAZIRI MEMBE ATEMBELEA BANDA LA WAJASIRIAMALI WANAODHAMINIWA NA UN

Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akinusa bidhaa ya mshumaa inayotengenezwa na wajasiriamali wanaodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilipofanya maadhimisho ya kusheherekea miaka 50 ya Uhuru jijini Dar es Salaam.Wa kwanza Kushoto  ni Mkurugenzi Mkuu wa J&L Handicrafts Louise Judicate Mushi na Katikati ni Mwakilishi UN Communication Group (UNCG) Magnus Michael Minja.
Waziri Membe akikagua bidhaa kwenye banda la Mama  Magessa Muna kutoka Kym's Enterprises.
Bi.Fatma Amour akionyesha zulia lililotengenezwa kwa ngozi ya Mbuzi kwa Mhe. Mgeni rasmi Waziri Membe.
Mgeni rasmi Mhe. Membe akizungumza na Programme Officer wa UNAIDS Amandine Oleffe katika banda la UNAIDS.

No comments: