UNAJUA KWAMBA MILLARD AYO ALIWAHI KUTOLEWA KATIKA CHUMBA CHA MTIHANI KWA KUTOMALIZIA ADA?
Kama
tulivyokuahidi msomaji wa Mo blog ifuatayo ni sehemu ya pili ya
mahojiano kati ya Mhariri wa Mo Blog Lemmy Hipolite na Mtangazaji
maarufu Millard Ayo.
Mo Blog: Tunamsikia Millard Ayo lakini hatujui ni nani hasa.?
Millard Ayo: Milliard
Ayo ni kijana wa miaka 26 aliyezaliwa tarehe 26 Januari mwaka 1986 ni
kijana aliyezaliwa katika hospitali ya Mount Meru na ni mtoto wa kwanza
kwenye familia ya watoto wanne.
Ninatoka katika familia ya Mzee Arael Ayo al maarufu kama ‘Chalii’ pale Tengeru mkoani Arusha.
Mo Blog: Tupe siri ya mafanikio yako pamoja na umaarufu ulionao.?
Millard Ayo: Kiukweli
moja kati ya vitu vinavyonifanya mimi nipate mafanikio, namshukuru
Mungu kwa sababu kwanza situmii vitu vinavyowaangusha watu wengi kwenye
kazi kama hizi; kwanza kabisa mimi sinywi pombe na sijawahi kunywa tangu
nizaliwe; nadhani inanisaidia pia kwa sababu wakati wote akili inakuwa
‘fresh’.
Mo Blog: Kwa kifupi tuambie ilikuaje mara ya mwisho tumekusikia Radio One ghafla Clouds FM.?
Millard Ayo: Clouds
Fm walivutiwa na kazi yangu, nadhani waliona uwezo wangu kupitia show
ya ‘Milazo 101’ niliokuwa nikiifanya Radio One so alinipigia simu bosi
wao nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumatano akaniambia tuonane.
Ukizingatia
mimi nilikuwa na dream sana kufanya kazi ‘Clouds’ hata wakati naingia
college ya Journalism nilikuwa na ndoto za kufanya kazi Clouds.
No comments:
Post a Comment