Monday, October 1, 2012

DAR LIVE ILIVYOBANJUKA JUU NA 'DNA' , WASANII WA BONGO JANA

 
DNA akiwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
 
…Akifanya makamuzi ya nguvu.
 
Dully Sykes akiwapa ‘hi’ mashabiki.
 
Roma akiwahamasisha mashabiki wake.
 
Jhikoman alipokuwa akitoa burudani ya Jumapili.
 
Jike la Simba, Isha Mashauzi, akiwajibika.
 
DNA akiwasilisha ujumbe kwa mashabiki.
 
Shadrack Joseph (mwenye suruali nyeusi) akicheza na kundi lake kibao cha marehemu Michael Jackson kiitwacho Thriller.
 
Rukia Juma ‘Mamaa Mashauzi’ akikamua na kundi la Mashauzi Classic.
 
Sehemu ya wanamuziki wa Mashauzi Classic wakiwa kazini.
 
Mkali wa sarakasi, Zungu Tasha, akifanya vitu vyake.
 
Shabiki ‘aliyeleta za kuleta’ akiondolewa na mabaunsa.
UMATI wa wapenzi wa burudani jana walibanjuka na msanii Denis Kaggia ‘DNA’ kutoka nchini Kenya katika onesho  lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.  Burudani hiyo ilisindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo mkali wa muziki wa reggae Jhikoman, Kundi la Taarab la  Mashauzi Classic, wanamuziki wa kizazi kipya, Shadrack Joseph, Roma, Dully Sykes na burudani ya sarakasi kutoka  mkali wa ishu hizo, Zungu Tasha.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments: