Wednesday, October 3, 2012

Heka heka za lala salama kuelekea kilele cha tamasha la serengeti fiesta 2012 mwembe yanga leo.




Mmoja wa watangazaji wa Clouds pichani kati,Antu Mandoza akiwa na baadhi ya washabiki wakubwa wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya viwanja vya Mwenge Yanga,Temeke jijini Dar mapema leo wakati heka heka za lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atatumbuiza.


Antu Mandoza,akimhoji Mwanadada Diana mara baada ya kujishindia kiasi cha shilingi 25,000/= pamoja na fulana ya fiesta mapema leo kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wakati heka heka za lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atatumbuiza.

Burudani ikiendelea kutolewa kwenye viwanja vya Mwembeyanga


Mmmoja washabiki wa tamasha la fiesta akizungumza kwa ufupi kuhusiana na tamasha hilo litakalorindima siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar.

Mtangazaji wa Clouds TV,kupitia kipindi cha Mwanadaisalama,Mussa Husein pichani kulia akiwauliza maswali baadhi ya watu kwa ajili ya kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa wakati heka heka za lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atatumbuiza.

Babu nae alikuwepo.

Kama ujuavyo panaposhughuli ya Fiesta kila mmoja hujipatia faida kwa namna moja ama nyingine












Mratibu wa kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mully B pichani kushoto akibadilishana mawazo na Mussa Husein,pichani kati ni dada Diana mkazi wa Temeke aliyejishindia fulana na sh 25,000/=


Bhaassss.

Panaposhughuli za Serengeti Fiesta huduma kama hizi hazikosekani,kuwajali wapenzi na washabiki wake kwa namna moja ama nyingine.

No comments: