Mgeni rasmi Kamanda wa kanda maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akimkabidhi cheti cha uanachama wa Fema Club Ivon John, Mkurugenzi mtarajiwa wa Flavour Media Company, katika mahafali yakuhitimu elimu ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari ya Kibasili yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo, Familia yako inakutakia maandalizi mema ya mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kuanza Oktoba 8 mwaka huu Mungu akutangulie ili uweze kufanya kwa utulivu na hatimaye upate mafanikio ya kuenedelea na kidato cha tano.
Kamanda Kova amewaasa wanafunzi hao kuwa na nidhamu katika masomo yao kwani nidhamu ndiyo inayozaa mafanikio yote katika maisha ya binadamu, usipokuwa na nidhamu hata ungekuwa na akili ya kiwango gani bila nidhamu utashindwa tu, na hautaweza kupata mafanikio yoyote.
Akaongeza na kusema "kwa sasa ajira ni ngumu hivyo msisome kwa malengo ya kuajiriwa someni kwa malengo ya kuwa wajasiriamali na kubuni zaidi shughuli za kufanya kuliko kufikiria ajira kwani hivi sasa wapo wasomi wengi ambao wako mtaani na digrii zao"
Kamanda Suleiman Kova akitoa nasaha zake kwa wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza elimu ya kidato cha nne wakati wa mahafali hayo shuleni hapi kulia ni kaimu mkuu wa Shule Mwalimu Masoi
Mgeni rasmi na meza kuu wakifuatyilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea katika mahafali hayo.
Ivon John akikata keki huku dada yake wa shule Hapy ambaye anaingia kidato cha sita mwaka ujao akimuangalia.
Mkurugenzi asiye na idara maalum Diana John akilishwa keki na dada yake Ivon John.
Mama Mkurugenzi akiwa na wakurugenzi katika picha.
Ivon John akiwa katika picha na shangazi ake kulia ni Shangazi Tusekile na kushoto ni Shangazi Neema.
Ivon akipozi kwa picha na zawadi zake.
Baadhi ya wanafunzi wa Kibasila wakiwa katika mahafali hayo.
Baadhi ya wazazi waliohudhuria katika mahafali ya watoto wao katika shule ya sekondari ya kibasila.
Vijana wa skauti kutoka shule ya sekondari ya Kibasila wakionyesha uwezo wao jinsi ya kupita kwenye kamba.
No comments:
Post a Comment