Saturday, October 20, 2012

KAPUMZIKE KWA AMANI MAREHEMU GIVELN ARBERT MWAMBAFU

 
Bw. Albert Mwambafu na mke wake wakiweka shada la Maua kwenye kaburi na mtoto wao mpendwa Marehemu Giveln Albert Mwambafu aliyefariki juzi baada ya kuugua ghafla na kupoteza maisha, Marehemu Givelin amezikwa jana kwenye makaburi ya Mbezi Tangi Bovu mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Tangi Bovu jijini Dar es salaam, Tunawapa pole wafiwa na mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mtoto wenu mpendwa marehemu Giveln.
"MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU GIVELIN MAHALI PEMA PEPONI AMEN"  
Jeneza la Marehemu Giveln likiwa tayari kwa mazishi mara baada ya kufika makaburini.
 
Mwili wa Marehemu Giveln ukiwekwa kaburini tayari kwa mazishi na kupumzishwa katika nyumba ya milele
 
Mwinjilisti Jane Kamugusha aliyeendesha ibada ya mazishi akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Giveln wakati wa mazishi jana.
 
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo nyumbani kwa Bw. Albert Mwambafu huko Mbezi Goigi.
 
Bw. Albert Mwambafu akiwa na majonzi makubwa pembeni mwa jeneza la mpendwa mtoto wake marehemu Giveln kabla ya kuingizwa kanisani tayari kwa ibada ya mazishi.
Mwili wa Marehemu Giveln ukiingizwa kanisani tayari kwa ibada ya mazishi.
 
Mwili wa marehemu Giveln ukiwa kanisani wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika jana kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach.
 
Waombolezaji wakiwa katika ibada hiyo.
 
Bibi wa Marehemu Mama Christina Mwambafu wa tatu kutoka kulia na waombolezaji wengine wakiwa na majonzi makubwa kwa kupotelewa na mjukuu wake
 
Mama wa marehemu Gilven Mwambafu Mrs Albert Mwambafu akilia kwa uchungu huku akisaidiwa wakati alipokuwa akiaga mwili wa mtoto wake mpendwa Giveln katika ibada ya mazishi iliyofanyika jana kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi , aliyesimama kulia nyuma ni Albert Mwambafu baba wa Marehemu.

No comments: