Thursday, October 11, 2012

LAPF YAKABIDHI MSAADA WA (SUN SCREEN LOTION) KWA CHAMA CHA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

 
Meneja wa kanda ya Kaskazini wa mfuko wa pensheni kwa wafanyakazi wa Serikaliza mitaa LAPF Bw. Lulyalya Sayi akikabidhi mafuta ya kulainisha ngozi kwa Ernest Kimaya Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za kanda Makumbusho jijini Dar es salaam, kulia ni Afisa Masoko wa LAPF Rehema Mkamba na kushoto ni Mweka hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdillah Omar.
 
Baadhi wa wanachama wa chama cha Albino Tanzania waliohudhuria katika hafla ya kukabidhi mafuta hayo
..............................................................
Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo umetoa msaada wa Lotion za Kuzuia Mionzi ya Jua kwa wanachama wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Dar es Salaam wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano.
LAPF inatambua madhara ya mionzi ya jua na pia umuhimu wa lotion hizi. inatambua pia mahitaji ni makubwa zaidi lakini kwa kuanzia imetoa msaada huu wa lotion 140 zenye ujazo wa 100 mls wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano ikiamini kwamba zitasaidia kupunguza mahitaji hayo. Kadhalika LAPF inawaomba msisite kuendelea kuwasilisha maombi hayo na itasaidia kadri uwezo utakavyo ruhusu.
LAPF imekuwa mstari mbele katika kusaidia makundi mbali mbali yenye ya watu wenye mahitaji maalum katika jamii hasa watu wenye ulemavu wa ngozi. Kama mtakumbuka mwaka juzi ilitoa msaada wa shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa boma kwa Mlemavu wa ngozi aliyekatwa mikono, mwaka jana tulitoa msaada wa fulana na vifaa mbali mbali kwa chama cha wenye ulemavu wa ngozi Dodoma na mwaka huu tukaona tuoe msaada huu wa lotion za kulainisha ngozi
Mtambue kuwa LAPF ni Mfuko wa Pensheni na wanachama wake ni mtu yeyote anaeamua kujiunga na LAPF iwe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe. Hifadhi ya jamii ni haki ya kila mtu hivyo tunawashauri ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi mjiunge na Mfuko huu unaotoa mafao bora zaidi nchini. Kadhalika LAPF imeanzisha mpango wa akiba wa hiari ambao unamfaa kila mtu na riba yake ni ya ushindani hivyo mjiwekee akiba kwa faida ya baadae.
Mbali na Mpango huo, LAPF inatoa Mafao ya Kustaafu, Mafao ya Warithi, Mafao ya Ulemavu, Mafao ya Uzazi na Msaada wa Mazishi kwa mwanachama aliyefariki. LAPF pia inatoa mikopo ya Nyumba kwa wanachama wanaokaribia kustaafu pamoja na mikopo ya wanachama kupitia SACCOS zao. Hivi sasa Mfuko uko kwenye hatua za mwisho kuanzisha Mafao ya Elimu.

No comments: