Jumuiya ya Commonwealth Countries
League (CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na nne (54) duniani kutoka
katika jumuiya ya madola iliandaa tamasha maalum siku ya jumamosi tarehe
3.11.12 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kumsaidia na kumwezesha
msichana kusoma elimu ya sekondari.
Historia
ya Commonwealth Countries League ilianzishwa rasmi kutoka kwa baadhi
ya wanawake mnamo mwaka 1923 nchini Australia kwa ajili ya kusaidia
kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume waliopo nchi
mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya ya madola.
Tamasha
hili lilifanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka
kwa Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa
jumuiya hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi Joyce Kallaghe. Wageni
Rasmi walikua Wastahiki Mameya wa Worshipful Royal Borough of
Kensington na Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na Mrs. Anne
Hobson
Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa
na wake za mabalozi kutoka katika jumuiya za Madola hamsini na nne (54)
ili kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza vitu mbalimbali vya asili kama
chakula, urembo, maua, vinywaji n.k. Fedha zote zilizopatikana
zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa
kike.
Aidha
Mama Balozi Joyce Kallaghe aliongeza kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa
Maisha kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima hivyo vipaumbele
vyote vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike walio
maskini au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa
kuendelea kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola".
Tangu mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa
kike 364 kutoka nchi 25 ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa
wazalendo kwa kuchangia mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com
Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka mzima
Asanteni
Urban Pulse Creative
No comments:
Post a Comment