Tuesday, February 11, 2014

MBUNGE DK. FAUSTINE NDUGULILE AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA BONANZA LA JOGGING & GLOBAL BREAKING NEWS DAR LIVE

Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Faustine Ndugulile, akiwa tayari kukabidhi tuzo kwa washindi wa bonanza hilo ndani ya Dar Live.
Bondia Hosen Nachoka wa klabu ya Kilimahewa Jogging, akipokea tuzo kutoka kwa Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, wakati wa Bonanza la Jogging & Global Breakingg News lililofanyika kwenye Uwanja wa Burudani wa Dar Live, juzi.
Bondia Mwina wa klabu ya Wembley akipewa tuzo na Mh. Ndugulile kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News lililofanyika Dar Live.
Bondia Mnyalu kutoka klabu ya Jogging ya Sheraton akijinyakulia zawadi kwenye bonanza hilo ndani ya Dar Live.
Mwakilishi wa klabu ya Magenge 20, akipokea tuzo baada ya timu yao kuibuka mabingwa wa netiboli kweney bonanza hilo.
Washindi wa pili katika mchezo wa soka kwa Maveterani, timu ya Mafaza Jogging Club wakijipatia zawadi yao katika bonanza hilo.
Bingwa wa soka kwa Maveterani, timu ya Sacramento Jogging wakipokea zawadi ya jezi seti moja katika bonanza hilo.
Mwakilishi wa klabu ya Azimio Jogging akipokea tuzo kwa timu yao kuibuka washindi wa pili katika soka la vijana kwenye Bonanza la Jogging na Global Breaking News, lililofanyika Dar Live juzi.
Mwakilishi wa klabu ya Sheraton Jogging, akipokea tuzo ya jezi seti moja kwa kuibuka mabingwa wa soka la vijana kwenye Bonanza la Jogging na Global Breaking News lililofanyika Dar Live juzi Jumapili.
(PICHA: ABDALLAH MRISHO / GPL)

No comments: