Tuesday, March 25, 2014

RIDHIWANI KIKWETE ATAKIWA KUWA MKALI KWA MAWAZIRI WASIOTOKA MAOFISINI KWENDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

1Mgombea Ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akimsikiliza mwanafunzi Asha Masoud wa shule ya msingi ya kijiji cha Makombe kata ya Lugoba. wakati alipofanya mkutano wa kampeni kijijini hapo, Ambapo amewaomba kura za ndio wananchi wa kijiji hicho ili aweze kutatua kero zao na kuleta maendeleo jimboni humo, Naye katibu wa NEC Itikadi, Siasa, na Uenezi (CCM) Nape nnauye akimnadi mgombea huyo amesema akishachaguliwa na kuwa mbunge wa Chalinze atatakiwa kuwa mkali kwa mawaziri. ili watoke maofisini na kwenda vijijini kusikiliza matatizo ya wananchi kama anavyofanya Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mwepesi wa kukagua miradi mbalimbali na kujua matatizo na kero za wananchi jambo ambalo linakuwa rahisi kuchukua hatua za utekelezaji, Uchaguzi wa jimbo la Chalizne unatarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu kuziba pengo la aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo, Kushoto ni Diwani wa kata ya Lugoba Bi. Rehema Issa Mwene.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LUGOBA -CHALINZE) 2Katibu wa NEC Itikadi, Siasa, na Uenezi (CCM) Nape nnauye kulia akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete katika kijiji cha Makombe kata ya Lugomba 3Diwani wa kata ya Lugoba Bi. Rehema Issa Mwene akimuombea kura Ridhiwani Kikwete kwa wananchi wa kijiji cha Makombe kilichopo katika kata yake ya Lugoba anayoiongoza. 4 Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akiomba kura kwa wananchi wa kijiji cha Makombe 5Kwaya ya uhamasishaji ikiimba katika mkutano huo 6Kazi ya kuchukua taswira nayo ni ngumu vijana wa kazi wakipozi kidogo kabla ya kuendelea na kazi hiyo. 7Sam wa Ukweli akitumbuiza 8Katibu wa NEC Itikadi, Siasa, na Uenezi (CCM) Nape nnauye akirika juu juu wakati akishiriki kucheza na Morani wa Kimasai 10Kundi la Fataki la TBC nalo limevamia chalinze kuanza kutoka burudani katika mikutano ya kampeni ya mgombea wa CCM Bw. Rhidhiwani Kikwete.

No comments: