Thursday, March 26, 2015

JEMBE FM YA MWANZA YAPEWA LESENI

DSC_0644
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni kwa redio ya Jembe FM ya jijini Mwanza kwenye ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa kurusha vipindi vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akikabidhi leseni kwa radio Jembe FM.
Alisema matumizi yasiyo sahihi yatasababisha mamlaka hiyo kunyang’anya leseni walioitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Alisema pamoja na haja ya kushiriki katika ushindani, kituo hicho kipya kinatakiwa kufuata masharti ya utangazaji ambayo yamo katika leseni waliyoiomba.
Alisema radio hiyo ya Mwanza inaongeza ushindani katika eneo hilo katika jumla ya radio FM 12 zinazosikika mjini humo, radio za kitaifa saba, za kikanda 11 na radio ya jamii 1.
Aliwataka kuwa waangalifu na kufuata kanuni za kitaalamua kufanyakazi wanasotahili za kuelimisha na kuburudisha.
DSC_0650
Alisema si radio tu ambayo ina nguvu ndiyo inayoweza kuhimili ushindani lakini pia ufuataji wa kanuni na maadili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk. Sebastian Ndege amesema kwamba wameanzisha radio hiyo kwa lengo la zaidi ya kuburudisha na kuelimisha bali kusaidia vijana kushika hatamu na kujitengenezea uwezo wa ajira.
Alisema kwamba ili kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kitaaluma wameajiri watu ambao wamesomea kazi husika ili kuhakikisha kwamba hawaendi kinyume na leseni yao.
Alisema kwamba wanaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kujaza mapengo ambayo yapo katika urushaji wa matangazo kwa sasa ili kuhudumia mji wa Mwanza ambao unakua kwa kasi kwa sasa.
DSC_0676
Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi (kushoto) akisisitiza jambo kwa uongozi wa JEMBE FM wakati wa hafla ya kukabidhi leseni kwa uongozi huo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam makao makuu ya ofisi za TCRA.
Alisema vipindi vyao vimezingatia haja ya jamii katika uchumi, elimu na afya.
Aidha amesema kwamba wanategemea kuwa na vipindi vizuri zaidi hasa kutokana na na uzoefu waliokuwa nao hasa wa uandaaji wa njia ya panda.
Jembe FM inamilikiwa na Jembe Media Limited.
DSC_0669
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk Sebastian Ndege (wa kwanza kushoto) na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited wakimsikiliza kwa makini kabisa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa leseni rasmi ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza.
DSC_0655
Baadhi ya wawakilishi wa kampuni ya Ndege Insurance inayomilikiwa na Dk. Sebastian Ndege waliojumuika kwenye hafla hiyo fupi.
DSC_0665
Maofisa mbalimbali kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo.
DSC_0683
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (kulia) akimkabidhi rasmi leseni ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege (katikati) katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya ofisi za TCRA jijini Dar. Kushoto ni Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi.
DSC_0712
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege akitoa neno la shukrani ambapo pia maeahidi kuwa atafuata masharti na kanuni zote zilizowekwa na mamlaka hiyo.
DSC_0725
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Jembe Media Ltd, Renata Ndege.
DSC_0733
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege na Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege wakionyesha leseni hiyo iliyoambatanishwa na miongozi ya Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria hafla hiyo.
DSC_0743

No comments: