¤Jumapili hii tarehe
03-May-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa atazindua
kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda mrefu mno.
¤Ni kitabu cha "Jifunze LINGALA kwa Kiswahili".
¤Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa sana la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner).
¤Ni ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili (03-May-2015) kuanzia saa 12 hadi
saa 3 jioni. MRC ndio ukumbi ambao "Club Raha Leo Show" ya TBC1 ilikuwa
inafanyikia.
¤Tshimanga Kalala Assosa amepata kupiga bendi nyingi
kubwa hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie),
Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu
na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Congo DRC. Kwa hapa Tanzania
amefanya kazi na Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre
Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis.
¤Mgeni rasmi wa tukio atatangazwa.
¤Wote mnakaribishwa. Wahi bila kukosa. Kiingilio ni BURE.
No comments:
Post a Comment