Monday, May 25, 2015

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WAFANYA MKUTANO

Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania ulioanza Mei 25-27, 2015 katika hoteli ya Ramada, Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo ni kujadili utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na mchango wa Wizara kufikia Dira ya Taifa 2025. Mkutano huu ni wa nne kufanyika tangu ule wa kwanza uolifanyika mwaka 1999 katika hoteli ya Whitesands, Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya mkutano ni Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025. Ujumbe huo umechaguliwa kwa kuzingatia mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika juhudi za kutimiza ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wa pili kutoka kushoto) akiongea wakati wa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania  ulioanza Mei 25-27, 2015 katika hoteli ya Ramada, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi Liberata Rutageruka Mulamula ambaye ameziwakilisha nchi za Marekani na Mexico ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi ambaye anawakilisha nchi za India,  Sri Lanka, Singapore na Nepal.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa Balozi Yahya Simba akitoa shukrani kwa viongozi waliweza kufanikisha mkutano huo.
Mabalozi wanaowakilisha Tanzania Nchi za Nje kutoka nchi mbali mbali wanaohudhuria mkutano huo.
Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbali mbali wanaohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini.

No comments: