KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.
Kesho, Ijumaa, Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
Vilevile, Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga. Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.

No comments:
Post a Comment