Wednesday, June 3, 2015

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA(TANAPA) KUPITIA UJIRANI MWEMA WAKABIDHI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA ASHIRA WILAYA YA MOSHI

Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Leonidas Gama akikaribishwa na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Erastus Rufungulo katika makabidhiano ya mradi wa maji wa ujirani Mwema uliotolewa na hifadhi za taifa nchni TANAPA.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika tanki la maji la mradi wa ujirani mwema uliotolewa na TANAPA kwa wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisoma kilichoandikwa katika vibao mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo.
RC ,Gama akinywa maji kwa kutumia mkono mara baada ya kufungua bomba la maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ashira katika wilaya ya Moshi ikiwa ni ishara ya kukabidhi mradi huo wa maji ulifadhiliwa na TANAPA kupitia mradi wa ujirani mwema.
Tanki la Maji la mradi wa ujirani mwema uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA).
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Erastus Rufungulo akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi wakati wa kukabidhi mradi wa maji wa ujirani mwema uliofadhiliwa na TANAPA.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Meneja Ujirani mwema wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania(TANAPA) Ahmed Mbugi akizungumza kuhusu miradi ya ujirani mwema ambayo TANAPA imekuwa ikiitoa kwa jamii katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ashira  katika wilaya ya Moshi .
Kaimu Mkurugenzi mkuu TANAPA,Ibrahim Musa akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi ,
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji uliofadhiliwa na TANAPA kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akiwahutubia wananchi waliofika katika makabidhiano ya mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi ,uliofadhiliwa na hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini, 

No comments: