Thursday, June 11, 2015

ASKOFU AWATAKA WATANZANIA WAJITOKEZE KUJIANDIKISHA

Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja (wapili kushoto) akiwa katika mahafali ya chuo cha Bibilia kinachomilikiwa na kanisa hilo.watatu kushoto ni Mgeni Rasmi Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa  Kanisa hilo Israel Maasa

Na woinde shizza ,Arusha
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church Eliud Isanja  amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo  ya taifa.

Isanja aliwaasa Watanzania kutozembea nafasi hiyo muhimu na badala yake waitumie fursa hiyo  itakayoleta  mabadiliko yanayotarajiwa na wengi.

Akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa Diploma ya masomo ya Biblia amesema kuwa Tanzania inahitaji Viongozi waadilifu na wenye bidii.
“Watu wasipige tu kelele barabarani bali wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoliongoza taifa hili” Alisema Isanja

Kwa upande wake Askofu Mwangalizi wa  Kanisa hilo Israel Maasa ambaye alikua mgeni wa heshima katika mahafali hayo amewataka watanzania kuwa makini na wagombea wanaowagawa Watu kwa misingi ya ukabila na udini na kutowachagua  kwani wataathiri umoja na mshikamano wa kitaifa.

Wilfred Pallangyo ameeleza kuwa ni wakati wa Watanzania kuwatambua viongozi watakaofaa kuliongoza taifa na kuwapa nafasi hiyo pasipokufanya makosa pia kuepuka vitendo vya rushwa hasa tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa  Tayari zoezi la uandikishaji limeanza katika baadhi ya mikoa na linategemewa kukamilika nchini kote  ili kukamilisha uchaguzi utakaoanza Octoba mwaka huu,vuguvugu la uchaguzi tayari limeanza tumeshuhudia hekaheka za wagombea wa Urais.

No comments: