Mapema wiki hii, mwanasanyansi wa kimataifa Mtanzania, mwanamama Dokta Mwelecele (Mwele) Malecela, alitangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa kuomba ridhaa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM. Dokta Mwele ambaye hadi wakati anatangaza uamuzi huo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ana historia ya kipekee ambayo nilibahatika kuifahamu kupitia chapisho moja lililopo katika blogu hii. Hata hivyo, chapisho hilo ambalo lilisomwa na maelfu ya watu, lilikuwa katika lugha ya Kiingereza. Makala hii ni marudio ya chapisho hilo kwa lugha ya Kiswahili. Maelezo hayo yanatoka mdomoni mwa Dkt Mwele mwenyewe ila mie nimetafsiri tu kwa Kiswahili.
Ajira yangu katika
Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ni hadithi ya bahati yenye
matokeo mazuri ambayo awali haikuwa katika nia yangu. Nilijiunga na taasisi
hiyo mwaka 1987 baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika stadi ya
wanyama na tabia zao (BSc in Zoology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
mwaka 1986. Baada ya usahili mzito, nilipangiwa kufanya kazi Kituo cha Amani
(Amani Centre), hususan kushughulikia ugonjwa unaofahamika kama Bancroftian
Filariasis. Nilishawahi kusikia kuhusu ugonjwa huo nilipokuwa mwanafunzi UDSM
chini ya uangalizi mzuri wa Mhadhiri Dokta Parkin lakini sikujua nini nitafanya
kuhusiana na ugonjwa huo. Kichwani mwangu, nilitamani kufanya kazi kuhusu
ugonjwa wa malaria ambao kwa wakati huo nilidhani ulikuwa eneo la kuvutia
kiutafiti. Kwahiyo, lazima Nikiri kwamba nilifadhaika kujikuta nashughulikia
ugonjwa wa Bancroftian Filariasis badala ya malaria, ambayo ilikuwa na nyenzo
nyingi kwa maana ya vifaa na ufadhili. Hata hivyo, niliambiwa bayana kuwa
lazima nishughulikie kufufua shughuli ya ugonjwa huo wa Bancroftian Filariasis
hapo Amani.
Nikiwa mtu ninayependa
kukabiliana na changamoto, nikaanza safari ndefu ya kupita Milima ya Usambara,
kuelekea sehemu hiyo inayoitwa
Amani.Safari ilikuwa katika mlolongo wa kupanda na kushika vilima kama mawimbi
vile hadi wakati flani sikuona watu wala makazi. Hofu yangu ilipunguzwa na
mandhari mazuri, misitu ya kupendeza, na hewa ilivyokuwa mwanana kadri
tulivyopanda milima. Nilipofika Amani, hofu yangu ilinirudia tena, nikijiuliza
iwapo ningemudu kweli kumudu maisha katika sehemu hiyo ambayo ilikuwa kama
mafichoni kwa wakati huo. Nilijifariji mwenyewe kwa kujikumbusha kwamba sehemu
hiyo tayari ilikuwa na wanasayansi kadhaa, na wamemudu kuishi hapo, Kwahiyo
nami ningeweza pia. Baba yangu alikuwa na msemo maarufu, ‘Ni juu yako kumudu
mazingira yanayokukabili,’ na hivyo ndivyo nilivyoamua kufanya.
Baada ya wiki
kadhaa za mafunzo ya kuelewa mazingira, hatimaye nilipangiwa kufanyakazi katika
maabara ya minyoo (helminthology laboratory) ambapo nilijifunza kuhusu
parasaiti aitwaye Wuchereria Bancrofti, ambaye ndiye anayeeneza ugonjwa wa
Bancroftian Filariasis. Nikajifunza kutambua hatua za awali za mzunguko wa
maisha ya parasaiti huyo na mwingine aitwaye Onchocerca Volvulus. Nikajifunza
kupasua mbu kwa ajili ya ucuhunguzi wa lava wa maambukizi na utambuzi wa mabara
wa parasaiti mbalimbali, kama vile wa kichocho (schistosomes), minyoo ya
tumboni (hookworks), trikurisi (Trichuris), nk. Wakati huo, dunia yangu ilikuwa
dunia ya minyoo, na watu walioniinghiza katika dunia hiyo walikuwa miongoni mwa
wajuzi wa mabara na wasaidizi wa mabara, ambao walinipatia mafunzo bora kabisa.
Nathamini mafunzo hayo kwa sababu yamesaidia sana kunifanya kuwa mtu niliye
sasa. Mmoja wa wasaidizi wa mabara alipendelea kunikumbusha kwamba alianza kazi
mwaka niliozaliwa. Haikujalisha walivyonichukulia kama mtoto, nilichukua kila
walichoniambia, na nilifurahia kila dakika. Kuna Nyakati familia yangu ilikuwa
na wasiwasi kuhusu maendeleo yangu.Niliwapigia simu zile za zamani za mkonga
kuwajulisha kuwa nilikuwa naendelea vema na kwa hakika ninapenda mahala hapo.
Kazi zangu za awali
zilijumuisha kuchunguza uhusiano kati ya parasaiti wa eosinophilia na helminth.
Pia nilichunguza matokeo ya majaribio ya maangamizi ya malaria katika
maambukizi ya Bancroftian Filariasis. Pia nilifanya kazi na marehemu Profesa
Chris Curtis kudhibiti mbu aina ya Culex katika mji wa Muheza kwa kutumia dawa
za kuua wadudu za polystyrene beads.
Baadaye nilikwenda
London, Uingereza kufanya Shahada ya Uzamili na ya Uzamifu katika Taasisi ya
Magonjwa ya Kitropiki ya Chuo Kikuu cha London, ambapo nilifanyia kazi
maambukizi ya filarial kwa paka. Paka hao walikuwa kwa ajili ya majaribio ya
uchunguzi ambao ulikuwa muhimu kwa uelewa wa maambukizi ya filarial. Kazi
niliyofanya ilikuwa kupata uelewa jinsi parasaiti wanavymudu kukwepa mfumo wa
kinga ya mwili wa kiumbe aliyeambukizwa, na matokeo ya uchunguzi wangu
yaligundua kuwa kuna molekyuli za
kiprotini (immunoglobulins) ambazo zilikuwa zikiwakinga parasaiti husika. Hii
ilisaidia kuongoza uelewa kuhusu watu wenye maambukizi ya filarial lakini
hawaonyeshi dalili za wazi.
Baada ya
kurudi nyumbani, nilijihusisha na kuandaa utafiti wa kuelewa kitu ambacho kwa
lugha ya kitaalam kinachoitwa immunoepidemiology ya maambukizi ya ugonjwa wa
mabusha.Utafiti huo uliofanyika Kingwende, Kenya na Masaika, Tanzania.
Machapisho kadhaa ya kitaaluma yalitokana na utafiti huo uliotuwezesha kufahamu
zaidi kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa mabusha, ambao ungetuwezesha kutafuta mbinu
bora za udhibiti.
Wakati huohuo,
nilihusika na kuandaa mpango wa kimkakati kwa ajili ya mradi wa kutokomeza
mabusha nchini Tanzania. Hii ilifuatiwa
na azimio la Shirika la Afya Duniani Mei 1997 ambalo lilisisitiza kuangamizwa
kwa ugonjwa huo.Uaandaji wa mpango huo madhubuti ulifuatiwa na kuteuliwa kwangu
kubwa mkurugenzi wa mradi unaohusu maradhi hayo mwaka 2000. Mwaka huohuo, mradi
wa kupambana na ugonjwa wa mabusha ulianzishwa katika kisiwa cha Mafia, na
mchango wangu kutoka maabara hadi kwenye eneo ambapo utafiti unatafsiriwa kwa
vitendo ulitimia kamili. Kuna msemo wa Kiswahili kwamba safari moja huanzisha
nyingine. Kwa upande wangu, hakujawa na mwisho wa safari hii bali ni vituo
tofauti tu ninaposimama kidogo lakini naendelea mwelekeo huohuo.
Mradi huo wa
kukabiliana na ugonjwa wa mabusha ulizidi kuimarika na sasa unafanya kazi
katika wilaya 53 na umewafikia watu MILIONI 13. Huku msukumo sasa ukiwa kwenye
magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika, njia zilizotumika katika mpango wa
kukabiliana na ugonjwa wa mabusha zimepanuliwa na kujumuisha ugonjwa wa
kichocho, minyoo wanaosambaa kupitia udongo na trakoma. Kwa kiasi kikubwa,
usaili wangu katika makao makuu ya NIMR uliniandaa kwa ajira ya utafiti na
udhibiti wa ugonjwa wa mabusha lakini kama ilivyo katika maeneo mengine ya
maisha, sikujua hilo kwa wakati huo. Nilipata fahari kubwa pale Rais Jakaya
Kikwete alipotangaza kuwa ataanzisha mfuko maalum kwa ajili ya ugonjwa huo
kuwasaidia watu wanaosumbuliwa nao. Rais alitoa tangazo hilo katika Mkutano wa
kimataifa wa masuala ya afya jijini Arusha, na hii imesaidia kupanua uelewa wa
madhila yanayowakabili wahanga wa ugonjwa huo nchini Tanzania na kwingineko barani
Afrika. Matokeo kutoka kituo cha uangalizi Tandahimba yanaonyesha mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha
umefanikiwa kupunguza maambukizi katika wilaya hiyo, na hiyo itakuwa sehemu ya
kwanza ya mafanikio ya kuingilia kati maambukizi kwa upande wa Tanzania Bara.
Je hii habari inayoelezea mafanikio? Ni habari
kuhusu binti mdogo aliyekuwa na ndoto za kuwa mtafiti; kuhusu msichana
aliyepanda vilima vya Amani kusaka ndoto yake, na ya mwanamke ambaye sasa
anaishi katika ndoto hiyo kwa kufanya tafiti na kuchangia katika kukabiliana na
ugonjwa ambao amekuwa akijishughulisha nao kwa takriban maisha yake yote. Labda
hayo ndio mafanikio. Au waonaje?
Nina deni kubwa kwa watu wengi walioniwezesha kufanikisha safari hii, hususan baba yangu Dokta John Malecela na marehemu Mrs Ezerina Malecela ambao walinihakikikisha kuwa "ndiyo, waweza kutimiza ndoto yako."
Hapa chini ni machapisho mbalimbali ya kitaaluma
Malecela M.N. Baldwin C.I and Denham D.A (1994) Hosts
antigen on the surface of microfilariae of Wuchereria bancrofti and Brugia
pahangi.
Transactions
Awarded prize for best presentation
Baldwin C.I., Medieros F, Malecela M.N. and Denham D.A
(1994) Humoral responses in cats repeatedly infected with Brugia pahangi.
Parasite 1,1S
Malecela (1995): Microfilariae and the immune response
in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Ph.D. thesis, University of
London.
P.E.Simonsen, D.W Meyrowitsch, W.G.Jaoko,M.N.Malecela,
D.Mukoko, E.M.Pedersen, J.H. Ouma, R.T.Rwegoshora, N.Masese, P.Magnussen, B.B.A
Estambale and E.Michael (2001) Bancroftian Filariasis infection,Diseaese and
Specific Antibody Response Patterns in a high and a low endemicity community in
East Africa. Parasite Immunology 23: 373-388
Michael E., Simonsen P.E., Malecela M., Mukoko D.,
Pedersen E.M., Rwegoshora R.T., Meyrowitsch D.W, Jaoko W.G., (2001)Transmission
intensity and immunoepidemiology of bancroftian filariasis in East Africa. Parasite
Immunology No 23. Pp 373-388
Paul Simonsen,Peter Bernhard, Walter Jaoko, Dan
Meyerowitsch, Mwele N.Malecela-Lazaro, Pascal Magnussen and Edwin Michael
(2002) Filaria Dance sign and subclinical hydrocele in two East African
communities with Bancroftian filariasis. Transactions of the Royal Society of
Tropical Medicine and Hygiene
Simonsen,P.E, Meyerowitsch, D.W, Jaoko W.G., Malecela,
M.N., Mukoko, D., Pedersen, E.M., Ouma,J.H., Rwegoshora, R.T., Masese.N
Magnussen, P., Estambale, B.B.A & Michael E. (2002) Bancroftian filariasis
infection disease and specific antibody responses patterns in a high and low
endemicity community in East Africa. American Journal of Tropical Medicine and
Hygiene Vol 66(5) pp550-559
Simonsen P.E Meyrowitsch D.W., Mukoko D, Pedersen
E.M., Malecela-Lazaro M.N., Rwegoshora R.T., Ouma J.H., Masese, N. , Jaoko
W.G., Michael E., (2004) The effect of repeated half-yearly mass treatment on
Wuchereria bancrofti infection and transmission in two East African communities
with different levels of endemicity. American Journal of Tropical Medicine and
Hygiene No 70 pp. 63-71
No comments:
Post a Comment