Thursday, June 25, 2015

KINANA AFANYA AMSHA AMSHA KUBWA JIMBO LA KWIMBA LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo katika Uwanja wa CCM, katika mji mdogo wa  Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uahi wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipohutubia mkutano wa hadhara aliofanya kwenye viwanja vya CCM kwenye mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo
 Wananchi waliofurika katikaUwanja wa CCM katika mji mdogo wa Ngudu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, abdulrahman Kinana alipowahutubia katika mkutano wake wahadhara uliofanyika kwenye viwanja hivyo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani Mwanza leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, uliofanyika leo kwenye viwanja vya CCM kwenye mji mdogo wa Ngudu wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Kwimba, Mansoor akihutubia mkutano wa katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo, kwenye Viwanja vya CCM, kwenye mji mdogo wa Ngudu, wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, magesa Mlongo, alipowasili kwenye Viwanja vya CCM, kwenye mji mdogo wa Ndugu, kuhutubia mkutano wa hadhara, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani humo,leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili katika Viwanja vya CCM, kwenye mji mdogo wa Ngudu, kuhutubiamkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo.
 Kinamama wakiwa na vyerehani ambavyo walikabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu aliufanya leo katika viwanja vya CCM katika mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo. vyerehani hivyovimetolewa na mbunge wa jimbo la Kwimba, Ndugu Mansoor

ALIPOWASILI KUANZA ZIARA KATIKA JIMBO LA KWIMBA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, wakati wa mapokezi yaliyofanyika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo. Kushoto ni Katibu wa  CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngesi.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa ngoma ya Sungusungu, wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo. Kushoto ni Katibu wa  CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngesi.
Katibu Mkuu wa CCM akivalishwa mavazi ya kiongozi wa Sungusungu, wakati wa mapokezi ya kuingia jimbo la Kwimba, yaliyofanyika  eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo hilo, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongoza msafara wa Sungusungu, wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo. Kushoto ni Katibu wa  CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngesi.
 Kinana akiwa rasmi Ki-Sungusungu
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akiwasalimia wananchi wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipowahutubia wananchi baada ya kupokewa katika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, na kufika Kijiji cha Hungumalwa, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo.Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Mbunge wa jimbo la Kwimba, NduguMansoor, akiwahutubia wananchi katika Kijiji cha Hungumalwa, mwanzoni mwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika jimbo la Kwimba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana  akiwahutubia wananchi katika Kijiji cha Hungumalwa, mwanzoni mwa ziara yake katika jimbo la Kwimba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasha taa kuzindua mradi wa umeme  katika kijiji cha Hungumalwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Cham katika jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma, alipowasili katika kijiji cha Hungumalwa,kushiriki ujenzi waZahanati katika kijiji hicho leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa chama, katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji cha Ilula, Amara Malelelemki, akitangaza kuhamia CCM, wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipozungumza na wananchi baada ya kuzindua ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Hungumalwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo laKwimba mkoani Mwanza leo.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akishiriki ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Hungumalwa, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipozindua ujenzi wa Zahanati hiyo, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza. Wapilikshoto ni Mbunge wa jimbo hilo, Ndugu Mansoor

KUMBUKUMBU MUHIMU YA MWALIMU NYERERE KATIKA WILAYA YA KWIMBA

 Jengo la Ofisi ya CCM wilya ya Kwimba mkoani Mwanza ambalo lilizinduliwa ujenzi wake na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere, tarehe 15/ 2/ 1975
 Wajumbe wakiwa kwneye Kikao cha Jimbo la Kwimba, ambacho Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikiongoza leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na Uhai wa Chama katika jimbo hilo mkoani Mwanza
 Katibu wa CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngwesa akitoa maelezo ya uhai wa Chama wakati wa kikao hicho cha jimbo kilichoongozwa na Kinana leo
 Mkuu wa wilaya ya Kwimba, Pili Moshi, akitoamaelezo ya Utekelezaji wa ilani ya CCM katika wilaya hiyo, wakati wa kikao cha jimbo la Kwimba, wakati wa kikao cha jimbo kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kulia), kilichofanyika ofisi ya CCM wilaya hiyo leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua mradi wa maji wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Mwanahamisi Pascal, baada ya kuzindua mradi wa maji wa Ngudu akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mbegu katika  kwenye vitalu ya uoteshaji miche ya miti, alipotembelea mradi wa Vijana wa Ngudu wa kutunza mazingira, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza leo
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akishiriki kupanda mbegu kwenye vitalu hivyo

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wauguzi na madaktari alipotembelea wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Adulrahman kinana akikagua chumba cha agonjwa mahututi alipotembelea wodi hiyo mpya katika hospitali ya mji mdogo wa ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani Mwanza
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye wakitoka kukagua wodi hiyo


NYUMBANI KWA BALOZI WA NYUMBA KUMI
 Mjumbe wa Shina namba 12, Spezioza Balele akifungua kikao cha Shina hilo, ambacho kilihudhiriwa na katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), katika Mtaa wa Ngumo kwenye mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo
Mjumbe huyo akimkaribisha Kinana baada ya kufungua kikao
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha shina namba 12, kilichofanyika nyumbani kwa Balozi wa shina hilo, Spesioza Balele, mtaa wa Ngumo, katika mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhaiwa chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments: