Thursday, June 4, 2015

MBUNGE JOSHUA NASSARI ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.



MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar jana ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Zoezi hilo lilo anza majira ya saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.
Akizungumza katika eneo hilo ,Nassar alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya kutoshja.

“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika ugali  na kazi ikaendelea”alisema Nassar.
Nassar aliwashukuru ijana zaidi ya 300 pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia moyo.


No comments: