Thursday, July 9, 2015

VILIO NA MAJONZI SINGIDA WAKATI MO AKIWAAGA WANANCHI WAKE!

IMG_7558
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.
Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB) wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.
Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo elimu na Afya
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo." alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini" alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1,000.
IMG_7562  
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema
Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida mjini.
Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza bungeni.
Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.
Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10, unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 81.
Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi chote!
IMG_7530
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza kutogombea tena.
Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba: "kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake, ikiwemo mimi mwenyewe."
Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.
"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.
"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! "
IMG_7549
Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake huku machozi yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.
IMG_7533
Watoto hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la ubunge wa Singida mjini.
IMG_7533 IMG_7535
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
IMG_7536 IMG_7567
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya People's Club.
IMG_7402
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa Singida mjini.
IMG_7588
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo.
IMG_7428
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake wakishambulia jukwaa.
IMG_7440
IMG_7445
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya Diamond Platnumz.
IMG_7447
IMG_7453
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika viwanja vya People's Club, Singida mjini.
IMG_7454
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
IMG_7471
IMG_7476
IMG_7478
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
IMG_7481
Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika katika viwanja vya People's Club kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh. Mohammed Dewji.
IMG_7610
IMG_7617
IMG_7626
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
IMG_7629
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
IMG_7642
IMG_7633
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa wananchi wa Singida mjini.
IMG_7645
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
IMG_7675
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
IMG_7712
Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
IMG_7716
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia) akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses Iyobo.
IMG_7728
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
IMG_7735
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.

No comments: