Tuesday, December 22, 2015

Diamond: Njooni Dar Live X-mas, sitawaangusha!

Funga Mwaka Concert 2015 (7)Funga Mwaka Concert 2015 (9)
Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (10)
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.

Funga Mwaka Concert 2015 (8)
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Funga Mwaka Concert 2015 (1)
Meneja Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (2)
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (3)Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.
Funga Mwaka Concert 2015 (4)
Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani mashabiki siku ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (5)
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Funga Mwaka Concert 2015 (6)
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Funga Mwaka Concert 2015 (18) Funga Mwaka Concert 2015 (19)
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Funga Mwaka Concert 2015 (20)
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (21)
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (22) Funga Mwaka Concert 2015 (23)Mashabiki wakiwa wamezingira gari la Diamond wakati akiondoka.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaahidi shoo ya nguvu mashabiki wake na kuwataka waje kwa wingi katika shoo kali ya kufunga mwaka itakayopigwa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar katika Sikukuu ya X-mas na kuwa hatawaangusha. 

 Diamond anayetamba na ngoma ya Utanipenda ameyaongea hayo leo kwenye mkutano maalum uliofanyika Karume, Dar ambao ulihusisha waandishi wa habari na wapenzi wa muziki kwa ajili ya kuzungumzia shoo hiyo kubwa kuliko inayojulikana kama Funga Mwaka Concert. 

 “Itakuwa ni Sikukuu ya Krismasi, sasa kwa nini tusifurahi pamoja, kama MTV wameamua kunipa tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika kwa hiyo sihitaji kuongea sana shoo itakuwaje siku hiyo, naomba mje kwa wingi kwa kweli sipendi kuwaudhi, nawaahidi sitawaangusha,” alisema Diamond au Baba Tiffah. 

 Pia waandaji wakuu wa shoo hiyo, Global Publishers Ltd, kupitia kwa Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, naye alizungumza machache pamoja na kutambulisha listi ya wasanii wengine watakaoambatana na Diamond siku hiyo. 

 “Mbali na Diamond pia kutakuwa na Msagasumu, Wakali Dancers, Staric pamoja na burudani nyingine nyingi. Haitakuwa shoo ndogo, Diamond ameamua kufurahi na mashabiki wa muziki siku ya Krismasi kwa kufunga na kuukaribisha mwaka mpya. 

Shoo zitaanza asubuhi kwa watoto mpaka saa 12 jioni kisha baada ya hapo ni watu wazima mpaka alfajiri,” alisema Mrisho. 

 Viingilio ni Sh 15,000 na kwa V.I.P ni Sh 30,000 lakini wadhamini wakuu wa shoo hiyo, Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel wakaamua kutoa ofa ya punguzo la bei kwa tiketi 1,000 za awali kwa watakaokata kupitia kadi mpya za Airtel Money Tap Tap zenye mfumo mpya wa kulipia bili mbalimbali. 

 “Kadi za Tap Tap zinazorahisisha kufanya malipo zaidi popote ulipo bila ya gharama yoyote tayari zipo zinapatikana maeneo ya Temeke na Ilala lakini kuwa nayo unapaswa kuwa na kadi ya Airtel na kwa wateja 1,000 wa kwanza wenye Tap Tap watakaokata tiketi kupitia kadi hiyo watakuwa na punguzo la Sh 5,000 yaani kwa 15,000 itakuwa 10,000 na 30,000 itakuwa 25,000,” alisema Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde. 
  Habari: Hans Mloli, Picha: Musa Mateja

No comments: