Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar. Kidoa (katikati) akiwasalimia mashabiki baada ya kutangazwa mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl
2015....Akilia kwa furaha.Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, Fatuma Makame....Akibusu tuzo. Akiwa katika picha ya pamoja na mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima (kulia).
2015....Akilia kwa furaha.Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, Fatuma Makame....Akibusu tuzo. Akiwa katika picha ya pamoja na mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima (kulia).
Mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015, Kidoa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Gazeti hilo.
Mwandishi wetu
Fainali ya lile Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 ilifanyika jana ambapo Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ aliibuka kidedea.
Kidoa alitangazwa mshindi kufuatia kupigiwa kura nyingi na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa hivyo kuwafunika wenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’.
Akizungumza na Risasi, mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima alisema kuwa, ushindani ulikuwa mkubwa kwani wasanii wote walioshiriki walikuwa wakali ile mbaya.
“Kidoa amefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi. Atapokea tuzo, cheti pia atapewa ofa ya kutengeneza nywele kwenye saluni ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar kwa miezi sita pamoja na kufanyiwa shopping ya nguvu,” alisema Amran.
(PICHA NA RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA/GPL)
No comments:
Post a Comment