Thursday, December 24, 2015

Pata punguzo la tiketi za Diamond Dar Live

mpya diamondMwandishi wetu KAMPUNI ya simu za mkononi, Airtel kupitia huduma yao ya kijanja kimawasiliano ya Airtel Money Tap Tap wanakuletea punguzo la bei za tiketi za kumshuhudia staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Krimasi (kesho) ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar. Akizungumza na Amani, Meneja Huduma wa Airtel, Moses James alisema kuwa mteja anatakiwa kununua laini yake ya Airtel kisha kujiunga na huduma ya Airtel Money Tap Tap na baada ya hapo atakabidhiwa namba ya siri ambapo ili kuanza kutumia huduma hiyo rasmi ni lazima mteja aweke kiasi cha kuanzia shilingi 11,000. “Watoa huduma wetu wa Airtel wanatoa huduma hii katika matawi yetu yote na hata ukienda Dar Live utaipata. Siku ya shoo ya Krismasi unachotakiwa ni kuonesha kadi yako ya Airtel Money Tap Tap kisha utapunguziwa bei ya tiketi kuanzia VIP ambayo ni 30,000 utapata kwa 25,000, kawaida 15,000 utapata kwa 10,000,” alisema Moses.

No comments: