Saturday, December 19, 2015

SHIRIKISHO LA WANAFUNZI VYUO VYA ELIMU YA JUU WAJA NA MIKAKATI


 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Zainab Abdallah, akizungumza na waandishi wa habari, jana jijini Dar es Salaam, Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Daniel Zenda, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Luhende Luhende na Katibu wa Idara ya Elimu, Tafiti na Uongozi, Ally Hapi. (Picha na Bashir Nkoromo).


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu waandishi wa habari,
Kamati ya Uratibu ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Taifa, ilifanya kikao cha kawaida cha siku mbili, tarehe 17/12/2015 – 18/12/2015 katika Ukumbi wa

Mikutano Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.

Pamoja  na mambo mengine ya kiutendaji, kamati ya uratibu taifa imefanya teuzi mbali mbali na kutoa maelekezo ya msingi yakutekelezwa  yanayolenga katika kukabili changamoto mbali mbali zinazowakabili wasomi wa vyuo  vya elimu ya juu nchini wakiwemo wale wanaohitimu masomo yao. Changamoto hizo ni kama ukosefu wa ajira, uzalendo na maadili ya taifa,kushuka kwa ari ya kujitegemea pamoja na uwezeshaji wa vijana wanaohitimu vyuo kiuchumi.


“A”  UUNDAJI WA IDARA NA UTEUZI WA WAKUU WA IDARA
Ndugu wanahabari, kamati ya Uratibu ya taifa kwa mujibu wa kanuni imeunda idara tatu za kiutendaji na kuwaweka wakuu wa idara watakaoshika Idara hizo ili kuleta kasi ya uchapakazi wenye lengo la kuboresha huduma kwa wadau wa Shirikisho. Idara hizo ni kama ifuatazo;-
1.    IDARA YA ELIMU,UTAFITI NA UONGOZI
Idara hii itashuhulika na mambo yote yakuandaa ya uongozi,Elimu, Utafiti, Mikopo ya wanafunzi, kuibua fikira na mawazo mapya miongoni mwa wasomi pamoja kuandaa mikakati ya kuwapika wasomi kuwa na stadi za kujiajiri.
-    Katibu wa idara aliyeteuliwa ni;-
Ndugu  Ally Salum Hapi
2.    IDARA YA UWEZESHAJI
Idara hii itahusika na usimamizi na uandaaji wa semina na midahalo mbali mbali ya kuibua fursa za ajira,kuwafundisha wasomi wahitimu kujiajiri,stadi za kuanzisha na kusimamia biashara.
-    Katibu aliyeteuliwa kushika Idara hii ni ;-
Ndugu  Reuben kwagilwa
3.    IDARA YA NJE NA UHUSIANO WA KIMATAIFA
Ndugu Waandishi, shirikisho letu linao wadau wanaosoma vyuo vya nje na mashirika ya ndani na nje yanayofanya kazi na wadau wetu. Idara hii itasimamia kuimarisha uhusiano wa shirikisho na taasisi za wanafunzi za ndani na nje ya nchi
-    Katibu wa Idara aliyeteuliwa ni;-
Ndugu Daniel  Zenda.
“B” TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA
Ndugu waandishi, tatizo la ajira kwa vijana wanaohitimu Elimu ya Juu ni changamoto kubwa inayolikabili Taifa letu.
Idara ya wahitimu wa Elimu ya Juu nchini ni zaidi ya 45,000 kwa mwaka . hali inayosababisha taizo la ajira. Idadi hii ni kubwa na haiwezi kubebwa na soko rasmi la ajira pekee. Hivyo ni lazima iwekwe mipango madhubuti ya kukabiliana na changamoto hii.
Kamati ya uratibu ya taifa imefanya yafuatayo kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wasomo:-
i/ Kuuanzisha dawati maalum la ajira
Dawati hili litakua chini ya idara ya uwezeshaji ya makao makuu na litashughulika na kukusanya taarifa zote zinazohusu ajira, wahitimu wa vyuo na kutafuta taarifa za  fursa za mbalimbali za ajira zilizopo ndani na nje ya nchi.
Dawati litaandaa program za mafunzo ya ujasiriamali, kuanzisha na kusimamia biashara, kuunda vikundi vya kiuchumi na kuanzisha makampuni kama ambavyo ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoelekeza juu ya uwezeshaji wa vujana kiuchumi.
Kamati ya uratibu imefanya uteuzi wa waratibu wa dawati la ajira kama ifuatavyo:-
   Ndugu Masiga Gulatone:   Tanzania bara
   Ndugu Arafa Ali Hassan:   Zanzibar
C: KERO ZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Kumekuwapo na matatizo yanayojirudia katika eneo la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini, hali inayosababisha malalamiko mengi kutoka kwa wanafunzi. Serikali ya awamu ya tano imepanua wigom mkubwa zaidi wa mikopo katika mwaka huu wa masomo ambapo zaidi ya wanafunzi elfu arobaini (40,000)wamepata mikopo nchini. Pamoja na juhudi hizo, yako malalamiko ya ucheleweshaji wa mikopo kutoka bodi ya mikopo na baadhi ya wanafunzi wenye sifa kukosa mikopo.
Ili kupata suluhu ya namna bora ya kushughulikia tatizo hili, kamati ya uratibu imechukua hatua zifuatazo:-
i/ kuanzisha dawati maalum la mikopo
dawati hili litakuwa chini ya idara ya elimu, utafiti na uongozi ya makao makuu ya shirikisho na litahusika na kukusanya taarifa za hali ya mikopo nchini, kero mbalimbali zinazohusu mikopo na kuzitafutia majawabu stahiki kwa kufuatilia katika mamlaka husika ikiwemo bodi ya mikopo haraka na kwa kuleta matokeo yanayohitajika.
Kamati ya uratibu imefanya uteuzi wa waratibu wa dawati hili kama ifuatavyo:-
   Ndugu Frank malako: Tanzania bara
   Ndugu Mohammed Nyimbo: Zanzibar
C: MIRADI YA KIUCHUMI
Ndugu wanahabari, Shirikisho linatarajia katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano kujikita katika kuibua, kuanzisha na kusimamia miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo italisaidia Shirikisho na vijana wahitimu wa vyuo kujiajiri na kujikwamua kiuchumi. Hii ni katika kuendana na ilani ya uchaguzi inayoelekeza serikali kuweka nguvu zaidi kwenye kuwawezesha vijana kiuchumi.
Kwa kuzingatia hili, kamati ya uratibu taifa imeamua kufanya yafuatayo:-
i/Kuanzisha dawati la miradi (Projects Desk)
Dawati hili litakua chini ya idara ya uwezeshaji ya Shirikisho makao Makuu na litafanya kazi ya kukusanya mawazo ya miradi mbalimbali kutoka kwa wasomi, kuibua miradi ya kiuchumi na kusimamia utekelezaji wake wa hatua kwa hatua kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho.
Kamati ya uratibu imefanya uteuzi wa mratibu wa dawati hili kama ifuatavyo:-
   Ngugu Britu Burule
D: KUSHUGHULIKIA DIASPORA
Kwa kuzingatia kuwa wako wadau wa Shirikisho ambao wanasoma vyuo vya nje ya nchi yetu, kamati ya uratibu imeona upo umuhimu mkubwa wa kuwatambua na kuwawekea utaratibu wa kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa kuzingatia umuhimu huo, kamati ya uratibu imechukua hatua ifuatayo:-
i/ Kuanzisha dawati maalum la Diaspora.
Dawati hili ,litakua chini ya idara ya Nje na uhusiano wa kimataifa ya Shirikisho makao Makuu na litashughulika na kukusanya taarifa za wanafunzi wote wa Diaspora na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kamati ya uratibu imefanya uteuzi wa waratibu wa dawati hili kama ifuatavyo:-
   Ngugu Petro Magoti:  Tanzania Bara
   Ndugu Juma Faki Juma: Zanzibar
E: UANZISHWAJI WA DAWATI LA TEKINOHAMA
Kamati ya uratibu ya taifa imeanzisha dawati maalumu la Tekinolojia ya habari kwa ajiri ya kutengeneza mfumo mzuri wa utoaji na upokeaji habari wa Shirikisho Makao makuu. Majukumu ya dawati hili ni pamoja na kuboresha mfumo wa mawasiliano baina ya Shirikisho na wadau wake kwa kufungua akaunti mbalimbali za mitandao, kufungua kurasa mbalimbali na tovuti ya Shirikisho. Dawati hili litakua chini ya idara ya Elimu, Utafiti na Uongozi ya Shirikisho makao Makuu.
Kamati ya uratibu imefanya uteuzi wa waratibu wa dawati hili kama ifuatavyo:-
   Ndugu Baraka Wambura: Tanzania bara
   Ndugu Abdullatif Kadiri Musa: Zanzibar
F: KAMATI ZA KISEKTA
Ili kuimarisha ufanisi wa kazi za idara za uchumi, uenezi na uhamasishaji, kamati ya uratibu imeteua kamati zitakazowasaidia makatibu wa idara hizo kutimiza majukumu yaom kwa ufanisi. Makatibu wa idara husika watakuwa wenyeviti wa kamati hizo. Walioteuliwa ni hawa wafuatao:-
Idara ya uhamasishaji
Mariam Fundi
Khadija Taya (Keisha)
Wakati Mtulya
Nourat Saidi
Pius Mpweza
Idara ya siasa na uenezi
Shhabani Shabani
Alex Muhando
Luiza Mgonja
Asha Hassan
Khamana Ghadafi
Idara ya Uchumi
Abdullatiif
Imani Matabula
Mh. Salim Turki
Mh. Neema majura
Mh. Angela Kizigha
G: KALENDA YA KAZI
Kamati ya uratibu ya taifa, baada ya kupitia mpangokazi wa Shirikisho uliopitishwa na Mkutano Mkuu wa Shirikisho mwezi May ,2015, imeelekeza kuanza kutekelezwa kwa mpango huo mara moja kwa kuwekewa Kalenda maalumu ya utekelezaji ambayo itaainisha majukumu ya kila kiongozi katika kila ngazi kwa kipindi cha mwaka mzima. Kalenda hii itawezesha utendaji kazi wa kila kiongozi kupimika katika vipimo mvinavyoonekana kwa matokeo ya wazi.
KAMATI YA KALENDA YA KAZI
Kamati ya uratibu imeunda kamati maalumu ya makatibu wa Siasa na uenezi, Katibu wa Uchumi na Fedha na katibu wa Uhamasishaji itakayoongozwa na ndugu Ally Salum hapi kama mwenyekiti kwa ajili ya kutengeneza kalenda hiyo. Kalenda inapaswa kuwa tayari tarehe 28/12/2015.
H: AHADI YA SERIKALI YA ELIMU BURE (kidato cha I-IV)
Kamati ya uratibu ya Shirikisho taifa inampongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza haraka na kwa vitendo ahadi yake ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne nchini. Kamati imepokea kwa furaha taarifa ya serikali kutenga kiasi cha shilingi bilioni 131 kwa ajili ya kutekeleza ahadi hii muhimu.
Kamati inawaomba wale wote waliopewa wajibu wa kusimamia fedha hizo kutimiza wajibu wao kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kutimiza malengo yanayotarajiwa. Aidha, kamati inamuomba Mh. Rais kutokuwa na huruma na yeyote ambvaye kwa namna yeyote ile atafanya urasimu usio na tija kukwamisha utekelezaji wa ahadi hii au kufanya ubadhirifu wa fedha hizi.
I: RAI YA KAMATI KWAMA WAZIRI WA KAZI, AJIRA
Kamati ya uratibu inapenda kuwakumbusha mawaziri wa wizara ya Elimu na Ajira kuwa wana wajibu wa kujipanga vizuri ili kuanza kutekeleza ahadi ya Mh. Rais na ilani ya uchaguzi ya CCM kuhusu eneo la mikopo ya milioni 50 kila kijiji/mtaa na kuwawezesha vijana waliohitimu elimu ya juu na vyuo vya ufundi kiuchumi kupitia uanzishwaji wa vikundi na makampuni.
Aidha kamati inawaomba kuhakikisha kuwa watumishi wote wa umma wenye vyeti feki watafutwe, wachukuliwe hatua za kisheria kwani wamekaa katika nafasi ambazo hawastahiki kuwa nazo. Kamati inamuomba waziri wa Kazi kuhakikisha kuwa kazi zote za makapuni ya kigeni ambazo zinawezwa kufanywa na vijana wa hapa Tanzania waajiriwe watanzania na si wageni kutoka nje. Agizo litolewe kwa makampuni na taasisi zote kujitathmini kama kweli wanatimiza lengo hili kwa vitendo.
J: CHAGUZI ZA SHIRIKISHO
Kamati ya uratibuimeelekeza kufanyika kwa chaguzi zote za matawi na mikoa ambayo haijafanya chaguzi hizo ili kuziba nafasi za viongozi wanaomaliza muda wao. Ratiba ya uchaguzi ni hii ifuatayo:-
RATIBA YA UCHAGUZI
MATAWI
04/01/2016 – 10/01/2016         Kuchukua fomu
11/01/2016 – 13/01/2016        Kamati za siasa za matawi
14/01/2016 – 15/01/2016        Vikao vya seneti mikoa
16/01/2016 – 17/01/2016        Uchaguzi
18/01/2016                                 Taarifa ya uchaguzi kutumwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa uchaguzi
MIKOA
19/01/2016 – 22/01/2016    Kuchukua fomu
23/01/2016 – 24/01/2016    Vikao vya seneti mikoa
25/01/2016 – 26/01/2016   Kutuma majina kwa Mkurugenzi Mkuu wa Uchaguzi
27/01/2016 – 28/01/2016   Kikao cha Kamati ya Uratibu taifa
30/01/2016 – 07/02/2016   UchaGUZI
Muhimu
Chaguzi zote za mikoa zitasimamiwa na kamati ya uratibu ya taifa na chaguzi za matawi zitasimamiwa na seneti za mikoa.Fomu za mikoa zitatumwa kutoka Shirikisho makao Makuu.
Kamati ya uratibu imemteua ndugu Ally S. Hapi kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Tunawatakia herim ya Xmas na Mwaka mpya
Ahsanteni.
IMETOLEWA NA
IDARA YA SIASA NA UENEZI
SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU
19/01/2015

 Kutoka Kushoto ni, Mganwa Nzota- Katibu Uhamasishaji, Joseph Chitinka- M-NEC,  Hamid Salim Mhina ( Makamu Mwenyekiti- Shirikisho Taifa, Zainab Abdalla (MKT), Ally Salum Hapi (Mkuu wa Idara ya Elimu Taifiti na Uongozi, Luhende  Luhernde (Katibu Uchumi na Fedha)  Daniel Zenda (Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa,

No comments: