Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki wao Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam
Waimbaji wa Bandi ya Skylight, Leah pamoja na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka kwenye bandi ya Skylight.
Ukafika muda wa kuzungusha mduara na kuona nani mwenye kiuno kilaini
Waimbaji wa bendi ya Skylight, Joniko Flower na Sony Masamba wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Bamutu ya Kongo wakisakata rhumba kwa staili ya aina yake Joniko Flower na Sony Masamba wakionesha umahiri wao mbele ya mashabiki.
Waimbaji pamoja na wapenzi wa bendi hiyo wakiendelea kuserebuka.
Sam Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na wenzake ndani ya bendi ya Skylight.
Moja ya staili zinazobamba duniani kote hata Skylight Band wanaicheza na mashabiki wao.
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni.
Hapana chezea kabisa watu wenye mapenzi na bendi yao....Copy and Paste mpaka raha..!
Ukafika muda wa kujimwanga uwanjani hakika Skylight inakupa burudani ya nguvu
Sony Masamba akichana mistari kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku Suzy pamoja na Sam Mapenzi wakipiga back vocal.
Mwimbaji mkali kutoka Bendi ya Skylight, Bijal Valentine akishusha mistari ya kufa mtu mbele ya mashabiki wao waliofika kwenye kiota Cha Escape One Jumapili iliyopita huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kushoto ni Leah na kulia ni Suzy
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Waimbaji wa Bandi ya Skylight Suzy (kushoto) pamoja na Natasha wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Sony Masamba akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Sam Mapenzi na Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Hakika Skylight Band inatoa burudani ya nguvu sasa njoo wewe na yule uone mambo mapya kutoka kwenye bandi yako
Waimbaji wa Bandi ya Skylight wakiongozwa na Natasha(katikati) akiimba moja ya nyimbo zinazobamba hapa nchini Tanzania na hata nje ya nchi huku akisindikizwa na wasanii wenzake Suzy pamoja na Leah wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka Skylight Band #JustFollowTheLight.
Mwimbaji mkali, Mao Santiago akishusha mistari mbele ya mashabiki wa band ya Skylight huku akisindikizwa na Joniko
Hyper Man(HK) akitoa ratiba ya Skylight Band siku ya Alhamis ndani ya Maisha Basement huko ni kubang chini kwa chini na Band yako ya Skylight
Msimu huu wa sikukuu kuelekea Xmass na Mwaka mpya ni Skylight Band pekeee itakayokuburudisha, karibu leo.
No comments:
Post a Comment