Sunday, December 27, 2015

WAANDISHI WA HABARI WASAIDIA WANAVIJIJI NCHINI KUSIKIKA KUPITIA SAUTI ZAO


Mraghabishi mwalimu Revocatus Renatus ( kulia )  wa kijiji cha Unyanyembe mkoani  Shinyanga akihojiwa na mtangazaji wa Redio Free Africa Felista Kujirilwa wakati wa  kuandaa  moja ya vipindi vya redio vya Chukua Hatua. 

“Haijatokea hata siku moja mwandishi wa habari akaja huku kwa kweli. Hii ni mara yangu ya

kwanza kuona wanahabari katika kijiji chetu. Toka nimezaliwa sijawahi kumuona mwandishi wa habari kuja hapa na mimi nina miaka 70.”  Hayo ni maneno ya Mzee Titus Ndugulile mraghabishi wa kijiji cha Mwamala-B kilichopo kata ya Mwamala wilaya ya Shinyanga vijijini.

Kijiji hicho kina wakazi wanaokaribia 2,820 toka katika vitingoji vya Mwanundi, Igegu, Witasisa na Wela. Yeye ni mmoja kati ya waraghabishi 400 waliosambaa katika vijiji zaidi 180 vilivyopo katika mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga. Kundi hili la waraghabishi linawajumuisha wakulima, viongozi wa dini, madiwani, wenyeviti wa vijiji, walimu, wanafunzi, wanawake viongozi na wafugaji wanaofanya kazi na programu ya redio ya Chukua Hatua inayorushwa na redio Kahama FM, Faraja FM, na Radio Free Afrika.

Redio hizi zimeanza kufanya kazi na Chukua Hatua kuanzia mwezi Novemba 2012 zikiwa na
lengo la kutoa fursa na nafasi kwa waraghabishi kuwakilisha mawazo, shida na vipaumbele vyao kwa viongozi ili waweze kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi. Lakini pia kuongeza wigo wa vyanzo vipya vya habari kwa vyombo hivyo. Waandishi hawa walitambulishwa

Kwa waraghabishi kupitia mafunzo, ziara za ufuatiliaji na uwezeshwaji wa wananchi katika
kung’amua matatizo yao na kupendekeza njia ya kuyatatua. Mafunzo na ziara hizi zilikuwa zinafanywa mashirika ya ADLG na CABUIPA ambao ni washirika watekelezaji wa programu ya Chukua Hatua katika maana ya uwezeshaji wananchi.  Matukio haya ya mafunzo na ZA `WWW3ziara ndio njia ya kwanza iliyotumika kuwatambulisha na kuwakutanisha waandishi na waraghabishi katika vijiji wanavyotoka.   “ Huku ni l i k uwa si j awahi kufika ni mara yangu ya kwanza na kiukweli watu wamefunguka sana kuhusu matatizo yao. 

Kila mtu anataka kuongea nasi mambo ni mengi na watu wanahamu ya kupaza sauti z a o  n a  wa n a t a k a  k u s i k i k a , ”anafafanua mtangazaji wa Redio Free Afrika Felista Kujirilwa baada ya kutembelea kijiji cha Mwambasha mkoani Shinyanga. Waraghabishi hawa wamepatiwamafunzo yaliyowawezesha kutambua haki na majukumu yao katika kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii zao. Wameweza pia kuchukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na wanajamii wengine  katika maeneo wanayotoka ila walikuwa  wanakosa sehemu ambayo  wangeweza kupaza sauti zao zaidi tukiacha mikutano ya vijiji na kwenye midahalo wanayoiandaa.  Hivyo redio hizi zimeweza kutoa nafasi kwa waraghabishi nasauti zao zinasikika na viongozi wao wanasikia na kuchukua hatua stahiki. Kama anavyoelezea  mtangazaji wa Kahama FM William Bundala ambaye pia anajulikana kama Kijukuu na wasikilizaji wake. “Baada ya kutoa taarifa za nyumba kupata nyufa kubwa kutokana na milipuko ya baruti inayolipuliwa kwenye mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, mkuu wa wilaya ya Kahama ameunda kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo ili kuweza kulitolea maamuzi. Tunaendelea kufuatilia kujua nini kitatokea, kubwa ikiwa ni kulipwa fidia kwa wale ambao nyumba zao zimeharibika.”
  

Lengo mojawapo la program ya redio ya Chukua Hatua ni kuhakikisha kwamba viongozi na wenye dhamana wanachukua hatua kwa kusikiliza matakwa ya wananchi. “Tunawashukuru sana waandishi wa Kahama FM na hasa Kijukuu kwa kazi nzuri wanayoifanya. Kama wasingekuja hapa sidhani hata kama mkuu wa wilaya angeweza kumtuma mwakilishi wake kuja zungumza nasi. Tutaendelea kuitumia redio hii mpaka pale haki itapotendeka kwa viongozi wetu,” anaelezea Halid Abdu mkazi wa kijiji  cha Shenda wilaya ya Gombwe mkoani Geita.  Hii ilikuwa baada ya redio Kahama FM kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mkutano wa kijiji ulioamua kuwatoa viongozi wa kijiji kwa tuhuma za kutumia vibaya fedha zinazotokana na vitega uchumi vya kijiji; ikiwamo makrasha, wachimbaji wadogo wadogo na malori yanayobeba mchanga katika mgodi mdogo unaomilikiwa na kiijiji hicho cha Shenda. Baada ya habari hiyo kurushwa redioni mkuu wa wilaya alilazimika kumtuma Mkurugenzi wake kwenda katika kijiji hicho ili kuongea na wananchi kuhusu kilio chao. Makutano haya baina ya waandishi wa habari na waraghabishi

Haya yamewezesha redio kupata vipindi mbalimbali nje ya mambo ya  Chukua Hatua.  “Hapa pana stori nyingi tofauti za kufanya, tumeongea na huyu binti, maskini kumbe ameambukizwa virusi vya ukimwi na ametueleza mambo mengi yanayotokea pale njia panda ya Tinde. Inabidi tufike hapo ili tufanye kipindi cha TV  kuhusu tatizo la Ukimwi na jinsi mabinti wanavyojiuza,” anaelezea Regina Mwalekwa wa kituo cha TV cha Clouds alipotembelea kijiji cha Kitule. Si hivyo tu vipindi vingine vinatumika katika taarifa za habari na hasa mafunzo ya waraghabishi
hasa ya viongozi wa dini, lakini pia waandishi wa redio hizi wangeweza kurekodi sauti za wanawake pia kwa ajili ya vipindi vya wanaawake na maendeleo

 Lakini pia kuna taarifa ya habari baadhi ya matukio ambayo waraghabi shi  wameweza kuyaelezea yametumika katika habari na zinasomwa redioni mfano tukio la wananchi wa kata ya Dutwa kuiomba serikali kupitia wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kutoa semina juu ya sheria za ardhi kwa mabaraza ya ardhi vijijini ili kupunguza migogoro ya ardhi inayosababisha vifo.  Habari hiyo iliyotumika June 6 2013 saa kumi kamili jioni na saa tatu usiku iliandikwa na mwaandaaji wa vipindi vya Chukua Hatua wa redio Kahama FM William Bundala. Ambapo mmoja wa wanakijiji hao Masalu Lugodisha, wa mjini Bariadi amesema, kutokana Jumuia ya Afrika

Mashariki kuungana, thamani ya ardhi itakuwa kubwa hivyo ni bora serikali ikalijua hilo mapema na kuanza kuepusha migogoro kwa wananchi.  Mpaka jumla ya vipindi 53 vimerushwa na redio hii vikiwamo vipindi 5 vya TV katika kituo cha Clouds. Huku wasanii wa Chukua Hatua toka katika wilaya za Maswa, Kahama na Shinyanga vijijini wakijiandaa kuigiza vipindi vya redio baada ya kumaliza mafunzo yao mwezi wa Juni 2013. Lakini si hilo tu madiwani wa kata za wilaya ya Bariadi wamenufaika na vipindi hivi kwa kuelezea mambo waliyoyafanya katika maeneo yao ikiwamo kupata mrejesho toka wa wapiga kura wao ni kwa kiasi gani wameweza kutimiza ahadi zao na hivyo kujiwekea mazingira mazuri ya kuchaguliwa tena.

Walimu waraghabishi nao wameweza kuelezea mikakati na jinsi wanavyofanya kazi na wanajamii katika kujikomboa na ujinga. Mfano mzuri ni waraghabishi walimu wa wilaya ya Kishapu na hasa kata ya Uchunga.   Kwa sasa programu hii ina waraghabishi zaidi ya 350. Akishangaa jinsi program ya Chukua Hatua inavyozidi kukua mmoja Wa waraghabishi  waanzilishi wa mwaka 2010, Titusi Ndugulile wa kijiji cha Mwamala B mkoani Shinyanga alisema,

“Yaani siamini kama hiki kitu kimekuwa hivi aisee. Nakumbuka siku ile tulikutana pale kempasi ya Chuo Kikuu cha Ushirika tulikuwa watu 12 tu, lakini leo limekuwa dude kubwa kabisa. Na waandishi wa habari nao wanatutembelea wanatuhoji, wanaturekodi kwenye haya mashikolo mageni yao.

No comments: