Mwenyekiti wa Africa Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu akizungumza kuhusu mkutano huo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba katika mkutano huo.
Meneja Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi akitoa taarifa kuhusu matumizi ya mobile banking nchini.
Mkurugenzi mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkakati wa Jackson Group Ltd, Kelvin Twissa akitoa mada katika mkutano huo.
Kutokana na kukua kwa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi (mobile banking), Watanzania wametakiwa kutumia nafasi hiyo vizuri ili iweze kuwasaidia kukuza uchumi wao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku mbili unaozungumzia maendeleo ya sekta za fedha kwa kutumia mifumo ya huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu (Africa Digital Banking Summit), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema ni muda muafaka kwa Watanzania kutumia huduma hizo kwa ajili ya kujiongezea kipato.
Mshereheshaji wa Africa Digital Banking Summit, Chris Mauki
Alisema kupitia huduma hizo, Watanzania wanaweza kutuma nakupokea pesa kutoka maeneo mbalimbali hata ambayo yapo mbali na matawi ya benki hivyo wanaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwepo kufanya biashara kwa kutumia huduma hizo.
“Serikali imeunganisha nchi nzima na mkongo wa taifa na hii inawapa fursa watanzania kutuma pesa sehemu yoyote hivyo niwasihi watanzania kutumia kikamilifu nafasi hiyo ili kuboresha uchumi wao,” amesema Dkt. Kijaji.
Nae Meneja wa Mifumo wa Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi amesema huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu imekuwa ikizidi kukua siku baada ya siku tangu ilipoanza nchini mwaka 2008 na mpaka sasa kuna benki 30 ambazo zimejiunga katika mfumo huo ili kuwasogezea huduma wateja wake.
No comments:
Post a Comment