Monday, May 9, 2016

BENKI YA AZANIA YATOA MSAADA WA MILIONI 5 KWA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango (kushoto), dawa na
vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na  Antusa Lasway.
Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo.
Hapa ni furaha tupu kabla ya kukabidhi msaada huo.
Makabidhiano zaidi ya msaada huo ukitolewa
mwonekano wa maboksi yenye msaada huo baada ya kupokelewa.
Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa.
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto), akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi. Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway.
Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Ofisa wa benki hiyo, Valentina Chesama akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Wafanyakazi hao wa Bebki ya Azania wakiondoka Hospitalini hapo baada ya kukabidhi msaada huo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya Azania imetoa msaada wa dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 5 wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Amani Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo wakati wa kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara, Mwanahiba Mzee alisema kila mara benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kulingana na ratiba yao ambapo mwaka huu waliona ni vema msaada huo waupeleke Hospitali hiyo.

Alisema mwaka katika kusherehekea sikukuu ya wanawake waliona ni vema kutoa msaada hasa katika wodi ya wajawazito ukizingia kuwa sikukuu hiyo inawahusu.

"Tumetoa msaada wa dawa mbalimbali kama dettol, spiritis, mabomba ya sindano, micoprostol, vitamini k na nyingine nyingi pamoja na vifaa vya usafi kama vile mifagio, sabuni na dawa za mswaki" alisema Mzee.

Kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali hiyo, Francis Yango akizungumza wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Shadrack Shimwela aliishukuru benki hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia.

"Tunawashukuru sana Azania Bank Ltd kwa msaada wenu lakini tunawaomba muende mbele zaidi kama mtaweza mtujengee walau wodi ambayo itaingiza walau vitanda 30 na wodi hiyo muandike jina la benki yenu kwani changamoto kubwa tulionayo kwa sasa licha ya kuwa na vitanda vya kutosha tuna uhaba wa wodi" alisema Yango.

No comments: