Tuesday, May 3, 2016

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) YAKUTANA NA WADAU WAKE JIJINI MBEYA

Meneja wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini  (TIRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Hiraly Maskini akifungua Mkutano wa  wadau wa soko la Bima kutoka Mikoani ya Nyanda za Juu Kusini  (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya Mei 3 -2016 mkutano ambao unalengo la kujadili na kutambua changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wadau hao katika kutekeleza majukumu yao.(Picha Emanuel Madafa,Jamiimojablogu-Mbeya) 

Wadau wa soko la  Bima Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juuu Kusini,Mbeya,Iringa,Njombe ,Rukwa ,Songwe na Katavi  wakiwa katika umakini kufuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo ulioandaliwa na  Mamlaka ya usimamizi wa Bima Nchini Kanda ya  Nyanda za Juu Kusini  (TIRA).

Kaimu Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Mbeya Ndugu Victory Mleleu akichangia moja ya maada katika mkutano huo ulihusisha wadau wa soko la Bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) semina ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Mei 3 mwaka huu.

Mhasibu wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima  (TIRA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Kurenje Mbura akiwasilisha moja ya maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima ulioitishwa na Mamlaka hiyo ya (TIRA ) Mei 3 Mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya. 

Mmoja wa wadau wa soko la Bima Mkoani Mbeya  Ndugu Masterdy Luvanda akichangia maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima  ulioitishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)  katika Ukumbi wa Mkapa jinini Mbeya Mei 3 mwaka huu, ukiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazo kutanana nazo wadau hao sanjali na kupeana uzoefu katika sekta hiyo.

Picha ya Pamoja Meza kuu na washiriki wa semina hiyo.

No comments: