Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation na washirika wake zilizofanikisha zoezi la kambi ya Moyo kwa watoto iliyokuwa katika Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo imemalizika juzi.
Baadhi ya wageni waalikwa na Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia tukio hiulo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na maafisa wa taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation wakati wa hafla hiyo jana usiku Mei 6.2016, Jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia tukio hafla hiyo
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakifuatilia hafla hiyo Baadhi ya Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakifuatilia hafla hiyo.
Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto akitoa shukrani zake kwa namna walivyoweza kufanikisha kambi hiyo ya Moyo hapa nchini.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI),Profesa Mohamed Janabi akitoa shukrani zake kwa taasisi zilizofanikisha zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akiabidhi tuzo kwa mgeni rasmi, Mh. Dk. Kigwangalla kwa namna Serikali inavyothamini mchango wa taasisi binafisi hapa nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi katika kuthamini taasisi hiyo
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri akikabidhi tuzo kwa Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete , Dk Peter Kisenge akitoa cheti maalum kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi akipokea tunzo maalum kama mchango wa JKCI katika kuthamini na kuokoa maisha ya watoto hapa nchini.
Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto akitoa tunzo maalum kwa Viongozi wakuu waliofanikisha taasisi zao katika zoezi la kambi ya moyo hapa nchini
Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto akitoa tunzo maalum kwa Viongozi wakuu waliofanikisha taasisi zao katika zoezi la kambi ya moyo hapa nchini
Picha chini ni baadhi ya Madaktari waliokabidhiw vyeti vya shukrani:
Prof. Jameel Alata ambaye ni kiongozi wa Madaktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation akiwemo Ahmed Said Abri (kulia). Muongoza hafla hiyo akielezea machache namna ya shughuli ya kambi liivyoendeshwa
Picha ya pamoja ya madaktari na wageni waalikwa akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa hafla hiyo ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipiga picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Moyo . Mwenye kanzu nyeupe ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Sheikh Said Ahmed Abri, akifuatiwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo, Profesa Joom Joom na mwingine ni daktari wa magonjwa ya Moyo aliyeambatana na timu hiyo ya madaktari hapa nchini.
Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo, Profesa Joom Joom akielezea jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) namna walivyoweza kufanikisha Operesheni zilizofanyika hapa nchini hasa kwa watoto waliokuwa na matatizo ya Ugonjwa wa Moyo. Operesheni hiyo maalum ilifanyika kuazia Aprili mwaka huu na kumalizika mwezi huu wa Mei. Hafla hiyo imefanyika jana Mei 6.2016 Jijini Dar es Salaam (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Serikali kupitia WIzara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imepongeza juhudi za Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Kiislam ya hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn Islamic Foundation kwa juhudi zake za kuunganisha nguvu na taasisi zingine za nje katika kuokoa maisha ya watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.
Akizungumza wakati wa hafla maalum ya kufunga kambi ya Moyo Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inatambua juhudi za taasisi binafsi katika kusaidiana nazo hivyo kwa hatua hiyo, suala la magonjwa ya moyo ambayo awali yalikuwa yakitibiwa nje kwa sasa yatashughulikiwa hapa hapa nchini.
“Tunaishukuru taasisi ya Dhi Nureyn na taasisi zote kwa kushirikiana na taasisi ya JKCI, kwani zimeweza kusaidia kuokoa maisha ya watanzania ikiwemo kuokoa vifo ambavyo vingetokea kwa watoto wenye matatizo ya moyo.
Zoezi hili limeweza kuvuka lengo la asilimia 70. Kwa wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu hayo ya moyo. Tunaamini mwaka huu tukaongeza malengo, na tayari wameweza kufanya operesheni takribani 200. Hii ni misheni ya pili na kwa maana hiyo wameweza kuvuka malengo ya asilimia 70 yale tuliyowapa.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Na kuongeza kuwa, Awali kabla ya utaratibu wa JKCI, wagonjwa 250 walikuwa wanapelekwa nje kufanyiwa operesheni hizo za magonjwa ya moyo. Lakini kwa mwaka huu hata miezi sita bado haijafika, Wagonjwa zaidi ya 200 wameshafanyiwa hapa hapa nchi operesheni hizo. Kwa hatua hiyo wameweza kuvuka lengo la asilimia 70 na wanataka wafikie angalau wagonjwa 400 hadi 500 kwa mwaka” alimalizia Dkr. Kigwangalla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Dhi Nureyn, Sheikh Said Ahmed Abri alieleza kuwa, taasisi hiyo imekuwa kiungo kuzitafuta taasisi zingine za nje ya nchi na kuleta wataalam hao wa bingwa wa magonjwa ya moyo hapa nchini ni faraja kubwa kwa taasisi hiyo na Watanzania wote kwani imeweza kuokoa maisha ya watoto hapa nchini.
Miongoni mwa taasisi hizo zilziofanikisha kambi hiyo ya Moyo hapa nchini ni pamoja na Taasisi ya Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktai kutoka Saud Arabia, Taasisi ya RAF kutoka Qatar, Taasisi ya Dhi Nureyn (Tanzania) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Tanzania). Zoezi hilo la kambi ya magonjwa ya moyo ni la pili kufanyika hapa nchini likiwemo la kwanza la mwezi Mei mwaka jana (2015) na kufanikiwa kuwatibu watoto 66 wa Kitanzania ambao walipangiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na kufanya kuokoa mabilioni ya shilingi ya Serikali kwa ajili ya gharama za matibabu hayo.
“Tunaishukuru sana taasisi ya Muntada Aid, kwa kujali, kuthamini na kujitolea kufanya kazi hii iliyookoa maisha ya Watoto weyu. Pia iliyowaondoshea maumivu watoto na wazazi wao na kuwapa matumaini mapya ya maisha. Pia tunaishukuru Serikali ya Saud Arabia, Taasisi ya Jakaya Kikwete na Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla pamoja na washirika wetu wote wakiwemo Taasisi ya Al Akhlaaq na wanahabari na wote kwa ujumla pamoja na mdaktari wa hapa ndani. Nashukuru sana” alimalizia Sheikh Said Ahmed Abri wakati wa kutoa hutuba yake hiyo kwa wageni mbalimbali pamoja na madaktari hao.
Aidha, madaktari hao pamoja na taasisi zote zilizofanikisha zoezi hilo, zilitunukiwa vyeti na tunzo maalum kwa ajili ya shukrani.
Na Andrew Chale,Modewjiblog, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment