Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru
inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti,
(katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma
George Chikawe, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam Juni 23, 2016. Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafiti
unaonyesha Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi
yake ya uchumi na nidhamu.
David Saile Mnoti, Mwanasheria, czi |
NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
TAASISI
ya ushauri wa mambo ya Habari ijulikanayo kama CZI, imetoa utafiti unaoonyesha
kuwa katika kipindi cha miezi 8 ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
Watanzania wengiwanamkubali Rais na wanayo imani kubwa Tanzania itarudi kwenye “mstari’.
Watafiti
hao, ambao ni David Saile Manoti ambaye amebobea kwenye masuala ya Sheria, Juma
George Chikawe, yeye ni mtaalamu wa Teknohama, na Dotto Nyirenda ambaye
amebobea kwenye masuala ya Kidiplomasia, wamesma sambambana utafitihuo pia
wameelezea kuwa Rais Magufuli atakapopewa dhamana ya kukiongoza Chama Cha
Mapinduzi CCM hapo Julai 27 kwenye mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala,
ufanisi wake katika kuongoza nchi utaongezeka.
Kwa
mujibu wa wanazuoni hao, walisema utafiti wao ulifanyika nchi nzima na
walitumia njia ya kuwahoji watu papo kwa hapo, kuwahoji kwa kupitia simu au
kuwahoji kimakundi.
Akizungumzia
utafiti wa miezi 8 ya Rais Magufuli akiwa madarakani, Mwanasheria David Saile
Manoti, alsiema, kundi la kwanza walilolihoji ni lile la vijana wenye umri kati
ya miaka 14-18 ambao wengi wao ni wanafunzi. “Baada ya kundi hili kuhojiwa
lilionyesha imani kubwa ya Rais kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, atarejesha
nidhamu ya masomo mashuleni.” Alsiema Manoti.
Kuhusu
kundi la vinaja wa miaka 10-30 asilimia 82 ya waliohojiwa wameonyesha imani
kuwa Rais John Magufuli ataleta mageuzi kwenye elimu hususan masuala ya mikopo
ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kumaliza tatizo la mabweni wka
wanafunzi.
Akizungumzia
kundi la miaka 30-60, Manoti alisema, Watumishi wa umma wameonyesha imani kuwa
Rais Magufuli atarejesha imani kwa serikali kutokana na jinsi anavyoshughulikia
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Aidha
utafiti unaonyesha kuwa asilimia 89.0 ya kundi hili limeonyesha imani kubwa kwa
Rais kumaliza matatizo ya wazee kwa kuanza kuwalipa posho kwa mwezi.
Katika
utafiti huu, Manoti amebainisha kuwa umoja na mshikamano mongoni mwa Watanzania
utaimarika zaidi, vile vile kundi hili limesema Rais Magufulu anazidi kuwa
maarufu huku wapinzani wakionekana kupoteza umaarufu klutokana na kushindwa
kubuni mbinu mpya ya mapambanoya kisiasa. "Kwa ujumla wake Mh. Rais Magufuli anakubalika kwa asilimia 89% huku akiwapiku Edward Lowassa na Mh. Jakaya Kikwete ambao wao wamegawana zilizobaki, Mh. Kikwete asilimia 7% na Mh. Edward Lowassa akiwa na asilimia 4%.
Akizungumzia
mkutano mkuu maalum wa CCM, Mwanadiplomasia Dotto Nyirenda yeye amewaasa wana
CCM kutambua mambo 10 ambayo Rais Magufuli anatosha kuyasimamia.
Aliyateja
mambo hayo kuwa ni pamoja na rasilimali watu, rasilimali ardhi, majengo na
viwanja, wanazuoni wa kila taaluma, wafanyabiashara ndogondogo (machinga),
wanayabiashara, wanachama wanaozidi milioni 9, Mashabiki wake wanaozidi milioni
28.9, wakulima, wavuvi, na wafugaji, laini pamoja na “utajiri” huo, CCM haiwezi
kujiendesha na inategemea ruzuku kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa,
pamoja na wafadhili ambao wengine sio wasafi kwenye rekodi zao.
Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, czi
Juma
George Chikawe, Mtaalamu wa Teknohama CZI
No comments:
Post a Comment