Wananchi wakiangalia ajali ya Noah yenye namba za usajili T 359 DFQ iliyodaiwa kuacha njia na kuparamia daladala namba T 797 DEW eneo la Buza Njia Panda ya Kitunda jijini Dar es Salaam leo jioni. Katika ajali hiyo watu wawili waliokuwa kwenye Noah hiyo waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.
Daladala lililogongana na Noah hiyo likiwa eneo la tukio.
Wananchi wakiwa eneo la ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment