Saturday, July 2, 2016

Oriflame yazindua bidhaa zake mpya za vipodozi

OriflameMeneja Masoko wa Kampuni ya Oriflame Bi. Mary Riung akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Piyush Chandra wakionyesha moja ya picha jinsi mtumiaji wa bidhaa hizo zinavyoweza kumsaidia katika ngozi yake.
DSC_9144
Bi. Erica Davies wa kampuni ya Oriflame akitoa maelezo namna bidhaa hiyo inavyoweza kusaidia katika ngozi hasa zile zenye makunyanzi na muonekano uliozeeka.. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Piyush Chandra na kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Oriflame Bi. Mary Riung

DSC_9110 DSC_9133 DSC_9115
Wafanyakazi wa Oriflame na wadau pamoja na wanahabari wakifuatilia uzinduzi huo
DSC_9136 DSC_9155 DSC_9124 DSC_9177 DSC_9110 DSC_9170 DSC_9168 DSC_9193 rr U36-620x399 DSC_9221Wafanyakazi wa Oriflame na wadau wakifurahia wakati wa ukataji wa keki maalum ( Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Kampuni ya ORIFLAME imezindua bidhaa zake mpya kwenye soko la Afrika Mashariki ambapo vipodozi maalum vitakavyokufanya ngozi yako kuonekana yenye kukaa na safi wakati wote kwa ngozi imeingia dukani kwa sasa.
Bidhaa hiyo maalum ni ya kusaidia ngozi kung’aa ambapo watumiaji wa bidhaa za ngozi wameshahuriwa kutumia bidhaa hiyo kwani imetengenezwa kwa vitu halisi ikiwemo matunda,mimea na majani ya hasili na kufanya ngozi kuwa katika hali ya afya wakati wote wa matumizi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bi. Mary Riung amebainisha kuwa, bidhaa hizo zitasaidia watu wengi kwani zimetengenezwa kwa ubora.
“Bidhaa hizi ni nzuri kwani zitakufanya kuweka ngozi yako kuwa nzuri ikiwemo kuondoa makunyanzi, kuondoa madoa na kufanya kuwa na rangi moja usoni. Ni bidhaa bora na itapatikana kwetu pekee katika soko la hapa Tanzania na Afrika Mashariki” alieleza Mary Riung.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Piyush Chandra amebainisha kuwa, kampuni hiyo ambayo ilianzishwa tokea 1967 imekuwa ni miongoni mwa makampuni yanayofanya vizuri katika bidhaa zake na watu wengi wametokea kuipenda hivyo kwa bidhaa zao zote wanazotengeneza zimeendelea kuwa na ubora Duniani kote.
Miongoni mwa bidhaa zao ni pamoja na NovAge ambayo imetengenezwa mahususi kumfanya mtumiaji ambaye ngozi yake imeonekana kuzeeka na endapo ataitumia vipodozi hivyo vitamfanya kumuondolea hali hiyo na kuonekana safi kama kijana kwani inaondoa makunyanzi ndani ya kuanzia wiki 12 huku ikiwa imethibitishwa na wataalamu kwa kuongeza ‘collagen kwa asilimia 200.

No comments: