Monday, July 4, 2016

UN YASHINDA KWENYE MAONYESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa pili kulia) akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, (wa kwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya ushindi katika banda lao. Kulia Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa pili kulia) pamoja na Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa wakiwa na tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kipengele cha habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika banda lao. Kulia Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa pili kulia), Hoyce Temu (katikati) pamoja na Edgar Kiliba (kushoto).
Wataalamu wa mawasiliano na Uhamasishajii (Communications, Advocacy and Partnership-COAP) wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifurahia ushindi huo katika banda lao. Kutoka kushoto ni Edgar Kiliba, Hoyce Temu na Didi Nafisa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) katika picha ya pamoja na vijana wanaojifunza kazi 'Intern' katika ofisi za Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba (katikati) na Msafiri Manongi.
Wananchi wakisaini kitabu cha wageni katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijni Dar es Salaam.
Kijana Msafiri Manongi anayejifunza kazi 'Intern' (kushoto) wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini sambamba na elimu ya Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu kwa kijana mwenzake (jina halikuweza kupatikana) aliyetembelea banda UN kwenye maonyesho ya Sabasaba yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Kijana Msafiri Manongi anayejifunza kazi 'Intern' kwenye Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) (kushoto) akipozi na kijana mwenzake aliyetembelea banda la UN kujifunza shughuli mbalimbali za UN Tanzania na kujinyakulia zawadi ya tisheti.
Kijana Edgar Kiliba anayejifunza kazi 'Intern' katika kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania (kulia), akitoa elimu ya Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu kwa wananchi wanaoendelea kufurika kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akitoa maelezo ya kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa kwa Bw. Rehani Athumani wa NHIF (kulia) aliyetembelea banda la UN Tanzania katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kijana Edgar Kiliba anayejifunza kazi 'Intern' katika kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
Makamu wa Rais wa Powerline Technologies Limited, Bw. Tumu Kaisi (kushoto) akibadilishana uzoefu na Kijana Msafiri Manongi anayejifunza kazi 'Intern' (kushoto) wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akimbandika zawadi ya beji ya' HE 4 SHE' ya Shirika la UN Women katika kampeni ya kuhamasisha wanaume waweze kuwasapoti wanawake katika nyanja mbalimbali kwa mmoja wa wananchi wanaoendelea kutembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kushika kasi jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wananchi wakisoma vipeperushi na majirada mbalimbali katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mtoto akisoma moja ya vitabu vyenye michoro ya katuni ambacho kilimvutia akisome alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa na wazazi wake.
Mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba akifurahia zawadi ya tisheti yenye ujumbe mzito wa kukomesha ukatili wa kijinsia inayosomeka "FUNGUKA" Tumia malaka yako KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA. Kulia ni Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Zaidi Enterprises, Eng. Allen Kimambo katika picha na mabango ya Malengo ya Dunia (Global Goals) ambayo ni sehemu anayoyafanyia katika utekelezaji wa kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
Mtaalamu wa Mawasiliano Mwandamizi wa Ukanda wa Afrika wa Jhpiego, Bw. Charles Wanga akiwa na mabango ya Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu katika banda la UN Tanzania.

Mkutubi wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Harriet Macha katika picha ya pamoja na mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba.


Baadhi ya wananchi na familia zao waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa wakipiga picha na mabango ya Malengo ya Dunia (Global Goals) ikiwa ni kampeni ya Umoja wa Mataifa katika utekelezaji wa malengo hayo kwa kila nchi mwananchama wa Umoja wa Mataifa.



Watoto nao waliwakilisha Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu. Kulia ni Msafiri Manongi kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Vijana wanaojifunza kazi katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini 'Intern' Edgar Kiliba (kushoto) na Msafiri Manongi (kulia) katika picha ya pamoja na wananchi wanaotembelea banda la Umoja wa Mataifa kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika hayo nchini.

Shirika la Umoja wa Mataifa limenyakua tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika sherehe za uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na mgeni rasmi Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame na kupokelewa na Mkuu wa Masharika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez.

Umoja wa Mataifa umekuwa kinara wa kuelimisha wananchi, kupitia njia mbalimbali ikiwemo redio, magazeti mitandao ya kijamii na pia kushiriki katika maonyesho ya sabasaba kila mwaka kwa Zaidi ya miaka 6 na kwa miaka 5 mfululizo wamekuwa wakishinda tuzo hizo.

Umoja wa Mataifa mwaka huu umekuja na kampeni ya uhamasishaji wa Malengo ya dunia (Global Goals) na umuhimu wa watanzania kuyaelewa malengo hayo na kuwa mabalozi katika kuhakikisha malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) yanatekelezeka.

Banda la Umoja wa Mataifa linapatikana katika ukumbi wa Karume yanakoendelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu 'sabasaba' katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

No comments: