![]() |
DC-Longido,Mh Chongolo. |
Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Godfrey Chongolo amemtia ndani Mkandarasi anayejenga barabara ya Longido-Kitumbeine-Oldonyolengai Bw. Loserian Sokonei Mollel kutokana na uzembe na kutotimiza matakwa ya mkataba na kuwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo pamoja na wananchi kwa ujumla.
Wakizungumza na mtandao huu, wananchi wa kijiji cha Gelai Lumbwa wamepongeza uamuzi wa DC Chongolo kwa sababu unasaidia kuondosha na kutatua kero zanazowasumbua na kuwakwaza kwenye maisha yao ya kila siku. "Tulichoshwa na watu waliokuwa wakifanya mambo vile wanavyotaka wao. Kwa hakika hii ni awamu ya Kazi Tu, tunamshukuru DC na OCD na tunamuunga mkono" alisema Mesiaki Laizer.
No comments:
Post a Comment